MAJUKUMU YA KITENGO CHA BIASHARA
Tunaweza kugawanya majukumu ya kitengo cha biashara katika makundi manne,
kama ifuatavyo:-
(A)Urasimishaji wa Biashara: - kundi hili linajumuisha majukumu yote mahususi ambayo yanahusiana na utekelezaji wa Sheriaya Leseni za Biashara na 25 ya 1972 na sheria ya Leseni za Vileo ya Mwaka 1968. Sheria hizi ndizo zimekuwa zikiwekewa mkazo na ndio majukumu ya msingi ambayo kitengo cha biashara
kinafanya kwasasa.
(B) Ukusanyaji wa Mapato:- Ukweli ni kwamba Kitengo cha biashara, hasa baada ya kurejeshwa ada za Leseni za biashara, kimekuwa mkombozi wa Halmashauri zote. Vyanzo vingi vya pato la ndani (ownsource) kama vile Ada za Leseni,Ushuru wa Huduma, Mabango, Usafirishaji, Kodi za pango kwenye masoko
na minada vinachangia kwa kiasi kikubwa pato la ndani la Halmashauri.
(C) Takwimu na Taarifa: - kundi hili linajumuisha ukusanyaji, upokeaji na usambazaji wa takwimu muhimu za biashara na wafanyabiashara, viwanda, biashara za mipakani, mazao ya kilimo, miundombinu ya masoko, wajasiriamali na wamachinga, taarifa za fursa za uwekezaji katika sekta mbalimbali
n.k.
D) Uwezeshaji: - kundi hili linajumuisha shughuli zote za kutoa elimu na taarifa za biashara kwa wafanyabiashara, mafunzo ya ujasiriamali,
uwaunganisha na masoko na maonyesho ya biashara, utambuzi na uanzishaji wa maeneo ya kufanyia biashara, n.k.
Haki Zote Zimahifadhiwa