Wananchi Washiriki Zoezi la Usafi Kibaha
Wananchi na watumishi wa Manispaa ya Kibaha wameshiriki kikamilifu katika zoezi la usafi wa mazingira lililofanyika katika maeneo mbalimbali ya manispaa hiyo kwa lengo la kuboresha afya na mandhari ya mji.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Afisa Mazingira wa Manispaa ya Kibaha, Bw. Issa Mohamed, alishiriki katika Kata ya Maili Moja hususan katika Soko la Maili Moja A na B. Aliwahamasisha wananchi na wafanyabiashara kufanya usafi katika maeneo ya makazi yao pamoja na maeneo ya biashara ili kudumisha mazingira safi na salama.
Bw. Issa alieleza kuwa usafi wa mazingira ni jukumu la kila mwananchi na si la serikali pekee. Alisisitiza umuhimu wa kufyeka nyasi, kuondoa takataka na kusafisha mifereji ya maji hasa mbele ya majengo na kando ya barabara ili kuzuia mazalia ya wadudu na magonjwa.
Akihitimisha zoezi hilo, aliwataka wananchi kuendeleza utamaduni wa kufanya usafi kila siku, akisisitiza kuwa usafi ni tabia inayopaswa kujengwa na kudumishwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Top of Form
Bottom of Form
Haki Zote Zimahifadhiwa