Tuesday 18th, March 2025
@Kibaha Mji Makao Makuu
Na Innocent Byarugaba, Kibaha
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhe. Leonard Mlowe amewaongoza Madiwani na wataalam kukagua miradi yenye thamani ya Tsh.11,069,500,000.00 iliyotekelezwa katika robo ya kwanza kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020.
Miradi hiyo ni vyumba 2 vya madarasa shule ya msingi Visiga vyenye thamani ya tsh.25,000,000.00, Madarasa 2 yenye thamani ya tsh. 29,000,000.00 shule ya msingi Madina, Zahanati ya Msangani yenye thamani ya tsh.154,000,000.00 na Bungo shule ya Msingi inayojenga vyumba 2 vya madarasa kwa tsh.32,000,000.00
Miradi mingine ni ujenzi wa hospitali ya Wilaya yenye thamani ya tsh.1,500,000,000.00, Soko kubwa la kisasa lenye thamani ya Tsh.8,000,000,000.00, Vyumba 4 vya madarasa shule ya msingi Kidimu yenye thamani ya Tsh.50,000,000 na jengo la wajasiliamali lenye thamani ya tsh.170,000,000.00
Aidha, halmashauri inajenga machinjio ya kisasa kwa gharama ya Tsh.804,500,000.00, Zahanati ya Bokotimiza ambayo mpaka sasa imetumia kiasi cha Tsh.60,000,000.00, ujenzi wa bweni shule ya sekondari Mwanalugali na samani zake kwa tsh.180,000,000.00, ukarabati wa shule ya Msingi Mkoani uliogharimu kiasi cha Tsh.15,000,000.00 na ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa shule ya Msingi Maendeleo yenye thamani ya Tsh.50,000,000.00
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Omari Bura amewataka wataalam kuendelea kusimamia miradi hiyo kwa ukaribu ili iwe na tija kwa wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Jenifa Omolo amesema halmashauri hiyo imekuwa ikitekeleza miradi yake kwa kufuata ushauri wa kitaalam, Sheria, kanuni na taratibu zote ili kuhakikisha mradi unaotekelezwa unalingana na thamani ya fedha ili utumike kwa kizazi cha sasa na baadaye.
Ukaguzi wa miradi kwa robo ya kwanza ni kiashiria kuwa sasa tunaingia robo ya pili itakayotufikisha katikati ya mwaka wa fedha 2019/2020.
Haki Zote Zimahifadhiwa