Na.Byarugaba Innocent,Kibaha.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhe.Mussa Ndomba amelieleza baraza la Madiwani kuwa kwenye Mpango wa bajeti ya 2023/2024 jumla ya shule za Sekondari tatu na moja shule ya Msingi zitajengwa.
Baraza hilo limeketi leo Jumatano Februari 22,2023 kupitia na kuridhia mapendekezo ya bajeti kwa Mwaka wa fedha 2023/2024
Shule hizo zitajengwa kwenye Kata ya Mkuza shule moja ya sekondari,Kata ya Tangini shule moja ya Sekondari na Kata ya Kibaha zikijengwa shule mbili Msingi na sekondari ili kuwaondolea kero wanafunzi
Mhe.Augustino Mdachi wa Kata ya Pangani na Mhe.Leonard Mlowe wamewapongeza wataalam wa Halmashauri kwa kuandaa bajeti kitaalam na wametoa rai kwenda kuitekeleza kama ilivyopangwa
Haki Zote Zimahifadhiwa