MHE.NDIKILO ATEMBELEA VIWANDA KIBAHA MJINI
Na.Innocent Byarugaba, Kibaha
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Evarist Ndikilo amefanya ziara ya Siku Moja mwishoni mwa wiki kwenye Halmashauri ya Mji Kibaha kujionea namna viwanda vinavyozidi kujengwa ,Kuanza uzalishaji huku akifurahishwa na idadi kubwa ya ajira zinaZotolewa kwa vijana wa Kitanzania
Akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Assumpter Mshama, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Bi Jenifa Omolo na Kamati ya ulinzi na Usalama amefurahishwa na ujenzi wa Kiwanda cha Kairuki kinachotarajiwa kutengenza dawa za binadamu na Vifa tiba huku kikiwa na mtaji wa bilioni 3.9 za ujenzi pekee
Ndikilo ameisifu menejimenti ya Kairuki kwa kuamua kufanya uwekezaji mkubwa ndani ya Mkoa wa Pwani na kwamba wameunga mkono kwa vitendo hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli aliyoitoa hivi karibuni wakati akizindua magari 181 ya Bohari ya Dawa nchini MSD kwamba kwa kufanya hivyo wamepunguza kiasi cha 500 bilioni ambazo hutumika kuagiza dawa na vifaa tiba nje ya nchi
Aidha, Pamoja na Kutoa ajira zaidi ya 1200 kwa watazania, amesisitiza viwanda vyote kuujulisha umma wa watanzania na dunia kwa ujumla kuwa bidhaa zao zimezalishwa Kibaha kwani huo ndio ukweli wenyewe na si China ama Dar es Salaam kama wanavyoandika “haiwezekani bidhaa izalishwe Kibaha tukiwa tunaiona ikizalishwa halafu eti inaandikwa made in China, hiyo haikubaliki”alisema
Viwanda vingine alivyotembelea ni kile kinachoounganisha Matrekta ya Ursus ,Kiwanda cha kukoboa na kusaga na nafaka cha jogoo, Kiwanda cha kutengeneza nguzo za umeme kwa teknolojia ya kutumia Mchanga na Sementi, Kiwanda cha kutengeneza betri za vyombo vya Moto, Kiwanda cha kutengeneza vibania nguo pamoja na kiwanda cha KEDS kinachotengeneza sabuni za unga pamoja na Misumari huku viwanda vyote vikiwa na Mtaji wa Zaidi ya Bilioni 34
Hii ni mara ya tatu kwa Mkuu wa Mkoa kufanya Ziara ya kuvitembelea viwanda katika Halmashauri ya Mji Kibaha ndani ya miezi 6 na kwamba Vimeendelea kujengwa na kuzalisha kwa kasi huku vikileta tija kwa taifa na kuboresha maendeleo ya watanzania Kimaisha.
Haki Zote Zimahifadhiwa