BAADHI YA MAJUKUMU YA MKUU WA IDARA YA KILIMO/UMWAGILIAJI NA USHIRIKA MJI KIBAHA.
(TAICO)
Kuratibu upatikanaji/uhakika wa chakula na ongezeko la kipato kwa kaya za wakulima katika Halmashauri ya Mji Kibaha.
Kuandaa malengo ya uzalishaji mazao kulingana na mazingira ya Halmashauri
Kuandaa mahitaji ya pembejeo na zana, kusimamia upatikanaji na Matumizi sahihi.
Kuratibu upatikanaji wa chakula, Matumizi na hifadhi ya kipindi cha njaa
Kuhimiza Ushirika na kusimamia uendelevu wake kwa ajili ya kuboresha soko la mazao na kipato kwa wakulima
Kubuni na kusimamia utekelezaji wa miradi ya kilimo kwa kuzingatia bajeti, sheria na miongozo iliyopo
Kuratibu zoezi la uibuaji miradi kulingana na fursa zilizopo
Kushirikiana na jamii kuwezesha miradi iliyopo kuwa endelevu kwa manufaa ya jamii
Kuandaa mpango wa mafunzo kwa maafisa ugani na wakulima pamoja na wana ushirika ili kuhakikisha mbinu, matokeo ya utafiti na technolojia mpya zinawafikia wananchi na wanazitumia kuongeza tija katika mipango yao.
Usimamizi wa matumizi sahihi ya rasilimali za Idara ya Kilimo na Ushirika kwa kuzingatia mifumo ya Kimenejiment(Performance Management Sysyems, Strategic Plan, Manifesto) na maelekezo kadri yatolewavyo na viongozi.
Kuwezesha Matumizi sahihi ya Sheria/ sera/miongozo ya kilimo kwa lengo la kuongeza tija katika kilimo ambazo ni pamoja na:
- Matumizi ya Sheria ndogo ya kilimo
- Matumizi sahihi ya sera na Miongozo ya kilimo
- Matumizi sahihi Sheria mama zinazosimamia kilimo
Kusimamia utendaji kazi wa maafisa ugani wa kilimo waliopo Ndani ya Mji Kibaha.
Kuandaa na kuwasilisha taarifa kulingana na mahitaji ya mfumo wa utawala katika ngazi mbalimbali.
Imeandaliwa na
NJAU, J.M.
AFISA KILIMO- MJI KIBAHA
Haki Zote Zimahifadhiwa