Majukumu ya Afisa Elimu Msingi ni;
- Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo, Sheria na kanuni zinazoongoza utoaji wa Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi;
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu utoaji wa Elimu ya Msingi na Awali katika Halmashauri;
- Kusimamia na kudhibiti matumizi ya fedha za elimu kwa mujibu wa miongozo ya fedha za Serikali;
- Kuratibu upanuzi wa Elimu katika ngazi ya Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya Watu Wazima na Vituo vya Ufundi Stadi;
- Kufuatilia na kutathmini maendeleo ya elimu katika Halmashauri ili kutoa ushauri wa kitaaluma kuhusu utoaji wa elimu nchini;
- Kutayarisha na kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya elimu kila mwaka;
- Kuhakikisha kwamba shule zote zinainua ubora wa mazingira ya kujifunzia na kufundishia; katika Halmashauri.
- Kusimamia udhibiti wa nidhamu, wajibu na haki za walimu na wanafunzi;
- Kuratibu na kusimamia mitihani ya Darasa la Nne, Darasa la Saba, na Mitihani ya vituo vya Ufundi Stadi katika halmashauri kwa kushirikiana na uongozi wa Elimu Mkoa na Baraza la Mitihani la Tanzania;
- Kufuatilia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi wa Shule na kuishauri Halmashauri kuhusu mbinu za kuinua taaluma na michezo na ubora wa Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi;
- Kukusanya, kuratibu na kuchambua takwimu za elimu katika Halmashauri kwa ajili ya Mipango ya maendeleo katika ngazi ya shule, Halmashauri, Mkoa na Taifa;
- Kufanya kazi nyingine kama utakavyoelekezwa na Mkururgenzi Mtendaji wa Halmashauri.
Haki Zote Zimahifadhiwa