Halmashauri ya Mji Kibaha ni Moja ya Halmashauri Tisa (9) zinazounda Mkoa wa Pwani.
Kulingana na makadrio ya sensa ya mwaka 2012 kwa mwaka 2017 Halmashauri inakadriwa kuwa na wakazi 144,241 Wanaume wakiwa 70,334 na wanawake 73,907. Watoto chini mwaka mmoja na wajawazito wanaotegemewa ni 7,155, Chini ya miaka mitano ni 21,269, wanawake walio kwenye umri wa kuzaa ni 40,634.
HALI YA HUDUMA ZA AFYA
- Huduma za OPD ni miongoni mwa huduma muhimu zinazotolewa katika vituo vyetu vyote vya Halmashauri ya Mji Kibaha.
- 48.2% ya wagonjwa wote wa OPD waliokuja kupata huduma katika vituo vyetu vya Afya ni wa hudhurio la kwanza (New Attendance) ambao ni sawa n a wagonjwa 102,637
- 25.1% ya wagonjwa wa OPD wote waliokuja kupata huduma kwa mwaka 2016 walikuwa watoto waliochini ya umri wa miaka 5 (<5yrs).
- 12.6% ya mahudhurio ya wagonjwa wa OPD waliokuja kupata huduma walikuwa wazee umri zaidi ya miaka 60 (60yrs <)
- Idadi ya wagonjwa waliopatiwa Rufaa ya kwenda Hospitali ya Rufaa ya Tumbi iliongezeka kutoka 1367 (2015) mpaka kufikia 2287 (2016).
NB:
Idadi hii ilitokana na Hospitali Teule ya Tumbi kupandishwa hadhi ya kuwa
Hospitali Teuli ya Mkoa na kufanya huduma zote za OPD kuanzia ngazi za
Zahanati na Vituo vya Afya.
Haki Zote Zimahifadhiwa