MAJUKUMU YA IDARA YA UJENZI
IDARA YA UJENZI INA VITENGO (SECTION) TATU AMBAZO NI;
-BARABARA –MAJENGO
-UMEME NA MITAMBO
BARABARA
1. Kusimamia matengenezo ya barabara za mji ambazo ziko kwenye ufadhili wa benki ya dunia na kuzikabidhi TARURA baada ya matengenezo na muda wa matazamio kumalizika.
2. Kutoa ushauri juu ya ujenzi wa barabara na makaravati katika mitaa pale ambapo jamii inatumia nguvu zake,tukishirikiana na Meneja wa TARURA
MAJENGO
1. Kusimamia ujenzi wa majengo ya serikali na wananchi
2. Kutoa vibali vya ujenzi
3. Kukagua majengo yaliyojengwa na kutoa ushauri
4. Kusimamia sheria na taratibu za ujenzi mijini
5. Kuandaa michoro ya ujenzi wa majengo
6. Kuandaa makisio na gharama za ujenzi
UMEME NA MITAMBO
1. Kusimamia utoaji wa huduma ya umeme mijini
2. Kusimamia kazi za umeme zinazofanywa katika majengo ya serikali
3. Kufanya kazi za umeme katika majengo ya serikali
4. Kusimamia kazi zinazofanywa na Greda
5. Kuandaa michoro ya wingizaji umeme katika majengo ya serikali
6. Kuandaa makisio ya vifaa vya umeme kwa wateja wanaohitaji huduma hiyo.
7. Kutatua/kurekebisha matatizo ya umeme katika majengo ya serikali
Haki Zote Zimahifadhiwa