Kitengo kilianzishwa Rasmi Januari, 2013 Katika Halmahauri yetu kikiwa na Watumishi Wawili mmoja kiwa ni Afisa Habari na Afisa TEHAMA.
Kitengo hiki kimekuwa kikifanya majukumu ambayo yamegawanywa sehemu mbili kama ifuatavyo;
I. Habari na Uhusiano
- Kusimamia Sera, Sheria, Taratibu na miongozo inayotolewa na serikali juu ya
uendeshaji wa Mifumo, Miundombinu na vifaa vya Habari na Mawasiliano katika Halmashauri Kutoa Matangazo yote ya Kazi na- Miradi inayotekelezwa kwenye Halmashauri
- Kutoa Vijarida, Vipeperushi na Vitambulisho vya kazi kwa watumishi wa Halmashauri
- Kutangaza Vivutio vya utalii na Maeneo ya Uwekezaji ya Halmashauri kwenye Tovuti,
Runinga, Magazeti na Redio Kupiga picha za Matukio mbalimbali yanayotokea Halmashauri na Kuyahidhi kwa
ajili ya Kumbukumbu za Halmashauri- Kukusanya na Kuaandaa Habari za Halmashauri
- Kukusanya Takwimu Mbalimbali za Halmashauri
- Kukusanya habari za Halmashauri zilizochapishwa kwenye Magazeti mbalimbali
- Kukusanya na kutunza habari za mtandaoni zinazoihusu Halmashauri kwa kutumia
“Computer” Maalum.- Kuboresha mahusiano kati ya Halmashauri, Waandishi wa Habari na Wananchi.
II. TEHAMA
A. Sehemu ya Miundombinu (Hardware and Networks)
- Kusimamia Sera, Sheria, Taratibu na miongozo ya Kitengo inayotolewa na serikali juu ya uendeshaji wa Kitengo cha TEHAMA & Uhusiano.
- Kitengo kimekuwa na utaratibu wa kuratibu na kufanya matengenezo ya awali ya
Vifaa vyote vya mifumo ya Habari na mawasiliano kila robo ya mwaka wa fedha.- Kuichunguza miundombinu ya TEHAMA mara kwa mara na kuchukua hatua pale inapobidi
- Kutengeneza mpango wa matengenezo(Preventive na maintenance plan) kwa kila mwaka
wa fedha.- Kutoa taarifa na ushauri wa mara kwa mara kuhusiana na vifaa vya kielectronics
- Kutoa ushauri wa jinsi ya kuimarisha usalama wa vifaa na miundombinu
Kutoa ushauri bora na viwango kwa vifaa vya TEHAMA vinanyo nunuliwa, kufungwa na vinanyotumika kulingana na viwango vilivyowekwa na Serikali- Kutoa taarifa/ripoti na ushauri kuhusu utekelezaji wa mpango mkakati wa uendeshaji wamatumizi ya TEHAMA
- Kuhakikisha kuwa miradi unayolenga uendeshaji wa Serikali mtandao inatekelezwa
ipasvyo.B. Sehemu ya Mifumo ya Habari (Information Systems)
- Kusimamia Sera, Sheria, Taratibu na miongozo inayotolewa na serikali juu ya uendeshaji wa Kitengo.
- Kitengo kimekuwa na utaratibu wa kuwakumbusha mara kwa mara wakuu wa idara na Vitengo na watumishi wengine wote umuhimu wa kutumia vizuizi vya virus(Antivirus) katika Kompyuta zao na kuvinyuwisha mara kwa mara.
- Utaratibu wa kuwakumbusha na kufanya backup ya taarifa/nyaraka zilizopo kwenye
Kompyuta.- Utaratibu wa kutumia nywira(password) katika kompyuta na vifaa vingine vya kielectronics.
- Kusimamia na kuratibu kazi za kitaalamu zinazofanywa katika kitengo .
- Kutoa taarifa/ripoti mbalimbali kuhusu utekelezaji wa mpango wa maboresho ya programu tumizi na mifumo ya Habari(Systems upgrading)
- Kutoa ushauri na bajeti ya mpango wa usalama wa programu tumizi na mifumo ya Habari Kuweka mikakati ya kuhakikisha kuwa ubora na viwango vya programu tumizi na mifumo ya Habari inafuata miongozo iliyopo.
- Kuhakikisha kuwa Miradi inayo lenga uendeshaji wa Serikali Mtandao inatekelezeka.
Lauriano M. Mwalongo Innocent Byarugaba
Afisa TEHAMA Afisa Habari
Haki Zote Zimahifadhiwa