Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha tarehe 04/12/2025 imefanya Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika tarehe 29 Oktoba, 2025, wameapishwa rasmi zoezi lilioenda sambamba na uchaguzi wa Mstahiki Meya na Naibu Meya wa Manispaa ya Kibaha
Kufuatia uchaguzi huo Mhe.Dkt Mawazo Ginhu Nicas Diwani wa kata ya Tumbi kupitia CCM amechaguliwa kuwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kibaha kwa kupata kura 19 kati ya kura zote 19 zilizopigwa na Mhe. Aziza Adinani Mruma diwani wa viti maalum Sofu kupitia CCM amechaguliwa kuwa Naibu Meya kwa kupata kura 19 kati ya 19.
Zoezi la upigaji kura limesimamiwa na Bw. Moses Gerald Magogwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kibaha, amewataka kuhakikisha wanakuwa kiunganishi sahihi kati ya serikali na wananchi kwa kusikiliza changamoto zote za wananchi na kuzipeleka kwa serikali kupitia vikao vya Baraza la madiwani ili ziweze kutatulia na hatimae wananchi waweze kupata maendeleo.
Kuapishwa kwa madiwani, pamoja na kumchagua mstahiki Meya na Naibu Meya sambamba na kuunda kamati za kudumu za Halmashauri ni hatua ya kuanza kutekeleza majukumu ya baraza katika halmashauri kwenye kuwatumikia wananchi wa Manispaa ya Kibaha
Haki Zote Zimahifadhiwa