• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kibaha Town Council
Kibaha Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Kibaha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto
      • Ujenzi
      • Mazingira na Usafishaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mazingira na Mipango Miji
      • UKIMWI
      • Maadili
      • Ustawi wa Jamii
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Viombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Mstahiki Meya Manispaa ya Kibaha ataka utendaji uliotukuka

Posted on: December 4th, 2025

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Dkt. Mawazo Nicas, amewataka wakuu wa Idara na watendaji kuacha kufanya kazi kwa mazoea, na badala yake kuongeza uwajibikaji ili kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo.

Aidha, amewataka madiwani kuwa waadilifu na kutanguliza maslahi ya wananchi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa lengo la kuleta maendeleo ya kweli.

Dkt. Nicas ametoa kauli hiyo wakati akizungumza katika mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani, uliolenga kula kiapo, kuchagua Meya, Naibu Meya pamoja na wajumbe wa kamati za kudumu.

Alisema huu ni wakati wa watendaji na wakuu wa idara kujitathmini na kwenda sambamba na kasi ya maendeleo, ili kuhakikisha wananchi wanapata matokeo chanya na kuendelea kufurahia huduma wanazozipata.

“Wananchi wategemee kicheko. Tunamshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo, Mimi nitakuwa sauti ya wanyonge wasio na sauti, Kila Jumanne na Alhamisi nitatenga muda maalum wa kusikiliza kero za wananchi,” alisema Dkt. Nicas.

“Tumepewa dhamana ya kuwatumikia wasio na sauti. Mimi nahitaji kazi tu, sitaki rushwa,” aliongeza Nicas.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha Mjini, Mwl. Mwajuma Nyamka, aliwasihi madiwani na watendaji kuwa wamoja, kuonesha upendo na mshikamano katika utekelezaji wa majukumu yao.


Nyamka aliwataka kuacha yaliyopita, kuangalia yaliyo mbele na kusimamia kikamilifu utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na Ilani ya CCM ya 2025–2030.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon, alisema huu ni wakati wa matokeo na kuwasihi madiwani kuhakikisha wanaendelea kuleta tija na maendeleo kwa wananchi.

Katika mkutano huo, Dkt. Nicas alichaguliwa kuwa Meya wa Kibaha kwa kipindi cha miaka mitano, huku Aziza Mruma akichaguliwa kuwa Naibu Meya kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Wakati huohuo, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Dkt. Rogers Shemwelekwa, aliwakabidhi madiwani vishikwambi na vifaa vingine vya kazi kwa ajili ya kuanza rasmi safari ya uongozi wao.

Matangazo

  • Tangazo la Kazi Halmashauri ya Manispaa Kibaha November 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUND VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 02, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -MSAIDIZI KUMBUKUMBU II October 06, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mhe Dkt Mawazo Ginhu Nicas achaguliwa kuwa Mstahiki Meya Manispaa ya Kibaha

    December 04, 2025
  • Mstahiki Meya Manispaa ya Kibaha ataka utendaji uliotukuka

    December 04, 2025
  • Dc Kibaha akabidhi gari jipya Divisheni ya ardhi na Mipango miji, awataka maafisa ardhi kutatua changamoto za wananchi,

    December 01, 2025
  • Dkt Bashiru awaagiza watendaji wa mifugo Kuongeza bunifu, Tafiti na Thamani ya Mazao

    November 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

Mubashara Baraza la kwanza la Madiwani Manispaa ya Kibaha
Picha za Kutembea

Kiungo cha Haraka

  • Sheria Ndogo(Ushuru wa magari ya abiria na mizigo)
  • Barua Pepe
  • Uujazi wa Viwanja
  • Muundo Wa Kiuongozi Halmashauri
  • Dira na Dhamira ya Halmashauri

Kiungo Kinachohusiana

  • Mkoa wa Pwani
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Ofisi ya Raisi, Tawala za Serikali za Mikoa na Mitaa
  • Utumishi
  • Utumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Ramani Ilipo

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera za Siri
    • Disclamer
    • MMM
    • Sitemap
    • Huduma

Haki Zote Zimahifadhiwa