MAJUKUMU YA KAZI ZA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII
Idara kwa ujumla inalo jukumu la kushirikisha jamii katika suala zima la kuondoa umaskini kwa kuiwezesha jamii kubaini matatizo yao, kupanga mipango yao, kutekeleza na kutathmini utekelezaji wa shughuli zao, kwa kutumia rasilimali zilizomo kwenye mazingira yao. Ikibidi kushirikisha juhudi za wengine, zikiwemo za Serikali, wahisani mbalimbali, lakini ushiriki wa jamii yenyewe ni muhimu zaidi ili kuwaletea maendeleo endelevu.
- Kuratibu shughuli za wanawake na watoto
- Kutoa mikopo na kufuatilia marejesho kwa vikundi vya wanawake na vijana
- Kufanya maadhimisho mbalimbali
- Siku ya wanawake Dunuani
- Siku ya mtoto wa Afrika
- Siku ya Mtoto wa kike
- Siku ya UKIMWI Duniani
- Siku ya Familia duniani
- Kuhamasishaji wa Jamii katika utekelezaji wa Miradi ya maji
- Kufanya mikutano ya kuamsha ari kwa jamii.
- Kuratibu shughuli za Dawati la Malalamiko
- Kuratibu na Kusajili Asasi za kiraia
- Kuratibu wa shughuli za Vijana.
- Kuratibu uwezeshaji wa wananchi kiuchumi
- Kushughulikia masuala ya Kitengo cha Ustawi wa jamii
- Kuratibu shughuli za TASAF kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini
UTEKELEZAJI KIPINDI CHA ROBO YA TATU MWAKA 2017/18
Uwezeshaji wananchi kiuchumi
Pamoja na majukumu ya kawaida Idara imeweza kufuatilia marejesho ya vikundi 108 vya wanawake vilivyopewa mkopo na riba TShs. 279,950,000/= iliyowanufaisha wanawake 805. Vikundi imeweza kurejesha Tshs: 120,305,000/= sawa na asilimia 43. Vikundi vya vijana kupitia SACCOS vimepewa mikopo ya Tshs. 20,000,000/= na kuweza kurejesha Tshs. 12,000,000/= baki Tshs. 8,000,000/=. Jumla ya form 93 zimegawiwa za kujiunga na Program ya VIA- jiandalie ajira kwa kushirikiana na Taasisi ya ujasiriamali (TECC) Tanzania Entrepreneurship and Competative Centre. Idara pia imepokea Tshs 19,000,000 kwa ajili ya kuvikopesha vikundi 2 vya vikundi ya vijana vya Rabit Farm na Peace Fish production toka katika Mfuko wa Maendeleo ya Vijana (YDF)
Uratibu wa asasi za kijamii
Idara imeratibu na kusajili asasi za kijamii 86. Asasi hizo zimeweza kutoa huduma mbalimbali kwa jamii zikiwemo za;-
- Mafunzo Wahamasishaji 24 wa Afya Majumbani
- Hatua za upangaji wa Mipango ya Maendeleo kwa kadri ya miongozo ya Halmashauri watu 1800 (Ke 1100 na Me 700) wamefikiwa kwa njia ya vipeperushi
- Wanawake 65 wamepata mafunzo juu ya umiliki wa ardhi.
Uratibu wa viwanda
Idara imeendelea na uratibu na uhamasishaji wa uanzishwaji wa viwanda vidogo na vya kati. Hadi sasa takwimu za viwanda vidogo 88 zimekusanywa. Viwanda hivi vinajishughulisha na Ubanguaji korosho, utengenezaji wa sabuni, batiki, uchomeaji vyuma, usindikaji wa vyakula, kutengeneza grisi, viatu na vifungashio
Kuamsha ari kwa jamii
Zoezi la kuamsha ari limefanyika katika Mitaa 7 iliyopo katika Kata 5 yenye miradi ya ujenzi wa zahanati, madarasa na vyoo vya shule za msingi. Wananchi wanaonyesha kuwa wana ari ya kushiriki na kuchangia utekelezaji wa miradi yao.
Maadhimisho ya siku ya wanawake dunuani
Siku ya wanawake duniani mwaka 2018 imeadhimishwa katika Kata ya Kibaha, Mtaa wa Mwendapole A. Kauli mbiu ya mwaka 2018 ilikuwa, “Kuelekea Uchumi wa Viwanda: Tuimarishe Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji Wanawake Vijijini’’. Maadhimisho yaliambatana maonesho ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na viwanda vidogo na vya kati vya wanawake wajasirimali.
Uhamasishaji jamii miradi ya maji
Uhamasishaji jamii katika utekelezaji wa miradi ya Maji umefanyika ambapo jamii imeunda vyombo vya watumia maji (COWSO) katika maeneo ya Sofu, Kalabaka, Muheza na Kidugalo ambapo uchaguzi wa viongozi wa vituo vya kuchotea maji umekamilika na uchaguzi wa viongozi wa jumuiya wameishachaguliwa.
Uratibu wa dawati la malalamiko
Dawati la malalamiko limepokea malalamiko kumi (10) kutoka Serikali ya Mtaa wa Mkuza, Idara ya Ardhi ihusuyo migogoro ya Ardhi, Idara ya maji (DAWASCO) kutoka Mtaa wa Uyaoni na Idara ya Maendeleo ya Jamii kuhusiana na Ajira kwa Vijana Viwandani. Malalamiko 2 kutoka Idara ya Maendeleo ya Jamii na moja kutoka Idara ya Maji (DAWASCO) yamepatiwa ufumbuzi (yamekamilika) na yaliyobaki yapo kwenye vitengo husika yanashughulikiwa.
Uratibu wa shughuli za TASAF
Utekelezaji wa shughuli za TASAF kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini katika robo ya tatu 2017/18 umezipatia fedha kaya masikini (walengwa) 2,136. Lengo ni kuzipatia kaya masikini ruzuku ya masharti na ruzuku isiyo na masharti ambapo walengwa hupatiwa ruzuku ya miezi miwili miwili kati ya Tshs. 20,000 na Tshs. 70,000 kulingana na ukubwa wa kaya na idadi ya wanakaya.
Aidha baadhi ya walengwa wameonyesha kuwa na mafanikio kwa kuboresha hali za maisha yao ambapo wameweza kuanzisha biashara ndogondogo, ufugaji, kilimo na kuboresha maisha.
Imeandaliwa na
Leah Lwanji
Afisa Maendeleo ya Jamii Mji
Halmashauri ya Mji Kibaha.
Haki Zote Zimahifadhiwa