Halmashauri ya Mji Kibaha inaundwa na Baraza lenye waheshimiwa madiwani 21, watano (5) ni wa viti maalumu na 14 ni wa kuchaguliwa. Pia Halmashauri ina
waheshimiwa wabunge wawili wanao ingia kwenye vikao kwa nyazifa zao. Baraza la madiwani lina kamati za kudumu tano (5) ambazo ni Kamati ya Fedha na
Utawala,Kamati ya Mipango Miji, Kamati ya Huduma za Jamii, Kamati ya Maadili na Kamati ya Kudhibiti UKIMWI. Kuna tarafa mbili ambazo ni Kongowe na Kibaha.
Katika utendaji wakazi za kila siku Halmashauri inaundwa na idara 13 ambazo ni Maendeleo ya Jamii,Fedha na Biashara , Utawala na Utumishi, Mipango na Takwimu,
Elimu Msingi,Elimu Sekondari, Maji, Ujenzi, Afya, Usafi na Mazingira, Kilimo na Ushirika, Mifugo na Uvuvi.
Pia kuna vitengo Sita ambavyo ni Kitengo cha Ugavi, Sheria, Ukaguzi wa Ndani, Uchaguzi , kitengo cha Nyuki,na kitengo cha TEHAMA Habari na Mawasiliano.
Kuna kata kumi na nne (14) na mitaa sabini na tatu (73).
Majukumu ya Idara:
- Idara inamajukumu kama ifuatavyo;
- Kuajiri kwa kuomba vibali vya ajira utumishi makao makuu.
- Kupandisha vyeo watumishi .
- Kuthibitisha watumishi.
- Kushughulikia nidhamu za watumishi.
- Kusimamia na kuhakikisha mikutano yote ya kisheri na kikanuni inafanyika
- kushughulikia mafunzo ya kujengea uwezo watumishi, waheshimiwa madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa.
- Kutekeleza mazoezi ya kitaifa yanayo tolewa.
- Kusimamia ulinzi na usalama wa mali zote za halmashauri.
- kwa mwaka wa fedha 2015/2016 watumishi 642 Walipandishwa vyeo ikiwa ni kutoka idara zote na vitengo vilinyopo kwa kufuata stahiki za mtumishi.
Watamishi 36 walithibitishwa kwazini na katika masuara ya kinidhamu watumishi wanne (4) wamefukuzwa kazi kwa makosa ya utoro na watumishi 21 wameondolewa kwenye
mfumo wa malipo ya mshahara na taratibu za kinidhamu zinaendelea kwenye mamlaka yao ya kinidhamu ambayo ni TSC.
Kuanzia mwezi wa tatu 2016 idara imetekeleza zoezi la uhakiki wa watumishi hewa pamoja na uhakiki wa vyeti vya watumishi na sasa bado tunaendelea na zoezi la
uhakiki kila mwezi kabla ya kulipa mishahara. Pia idara kwa kutumia mfuko wa ULGSP na mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2015/2016 yametolewa mafunzo kwa waheshiwa madiwani kuhusu utwala bola, wenyeviti wa mitaa kuhusu uongozi ,kukusanya kodi za majengo pamoja na utunzaji wa mazingira na usafi,watumishi na wakuu wa idara na vitengo nao walipata mafunzo
mbalimbali.
Mkuu wa Idara: GEORGE P. MBOGO
Haki Zote Zimahifadhiwa