KAZI ZA AFISA BIASHARA WA HALMASHAURI YA MJI KIBAHA
Ili kufanikishwa mapinduzi ya Kiuchumi, Maafisa Biashara wanatakiwa kutekeleza majukumu kama yalivyoainishwa kwenye mwongozo Na CFB/173/355/01 wa tarehe 06/06/2011 kutoka WIZARA YA VIWANDA NA TAMISEMI kama ifuatayo:
- Kuratibu utekelezaji wa Sera, Sheria, na Kanuni na taratibu za Sekta za Viwanda, Biashara na Masoko katika Mamlaka ya serikali za Mitaa;
- Kutoa Elimu ya ujasiriamali kwa wafanyabiashara wadogo walioko katika sekta binafsi katika eneo lililo chini ya mamlaka .
- Kuwa kiungo na wizara kupokea taarifa za sera ,Seria na mikakati ya Wizara na kuzisambaza kwa wadau mabalimbali katika mamlaka za Serikali za Mitaa;
- Kupokea ,kuchambua na kuunganisha taarifa za usambazaji katika sekta ya viwanda, Biashara na Masoko na kutoa taarifa OWM - TAMISEMI,Wizara ya Viwanda na Biashara na kwenye Sekretariati za Mikoa na kushauri ipasavyo;
- Kushauri na kuratibu shughuli za usajili wa Shughuli za Biashara katika mamlaka za Serikali za Mitaa (Business Activities Registration) kwa mujibu wa sheria.
- Kupendekeza namna ya kuboresha mazingira wezeshi ya biashara kwa madhumuni ya kurahisisha taratibu za kuanzisha biashara nchini ;
- Kushauri namna ya kuikuza Sekta Binafsi kwa lengo la kuifanya ya ushindani;
- kuhamisha matumizi ya bidhaa ya Tanzania - (Buy Tanzanian Building Tanzania);
- Kuwasiliana na Wizara/Taasisi na mashirika yanayosimamia Sheria /kanuni za kufanya biashara ili kupata takwimu kwa ajili ya kutathimi mwenendo wa biashara nchini;
- Kuziunganisha Taasisi zilizo chini wizara na mamlaka za Serikali za mitaa (Mjiji,Manispaa, Mji na Halmashauri za wilaya) kwa lengo kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Taasisi hizo;
- Kutoa ushauri juu ya mifumo ya kuwakinga wakulima na madhara ya mabadilikoya bei (Commodity Price Risk Management) kama vile wa Stakabadhi Ghalani na kuhakikisha unapanuliwa kwa mazao yanazalishwa na wakulima katika wilaya na mkoa ili kuinua kinua kipato cha wakulima .
- kutoa ushauri juu ya dhana ya wilaya moja zao moja (one village,one product concept) kulingana na fursa zilizopo kwa kuzingatia (comparative and competitive advatage);
- Kuthamini mwenendo wa biashara kwa kuangalia hali ya masoko ,bidhaa zinauzwa katika masoko ,bidhaa zinauzwa katika soko la ndani na nje ya nchi na kuandaa chati ya kuonyesha hali ya biashara kwa vipindi vya robo nusu na mwaka ;
- Kutathimini mwenendo wa uzalishaji na biashara katika maeneo huru ya biashara (EPZ)na kushauri ipasavyo;
- Kuanisha bidhaa zinazoweza kuuzwa nje ya nchi (Export Potential ) na kutoa taarifa na ushauri kwa wadau ;
- Kufuatilia mwenendo wa uzalishaji katika viwanda na mauzo yake katika soko la ndani - Mikoa na wilaya mbalimbali ;
- kuratibu maendeleo ya biashara ndogo , kubwa sekta isiyo rasmi na kutoa taarifa OWM- TAMISEMI, Mikoa na Wizara ya Viwanda na Biashara;
- Kutathamini na kutoa ushauri kuhusu ubora wa huduma za viwanda biashara na Masoko zitolewazo na makampuni mabaalimbali;
- Kukusanya na kuchambua takwimu za mahitaji na usambazaji wa bidhaa nchini ;
- Kuratibu uwekezaji wa mikakati ya biashara kati ya nchi za Afrika Mashariki na Jumuiya nyingine ambazo sisi ni wanachama kama vile SADC;
- Kutoa mapendekezo ya kuboresha Sera za Sekta za Viwanda , Biashara na Masoko katika ngazi ya mamlaka za serikali za Mitaa na
- Kuratibu mikutatano ya Kisekta kwa kushirikiana na Wizara , OWM- TAMISEMI na Mikoa.
Haki Zote Zimahifadhiwa