• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kibaha Town Council
Kibaha Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Kibaha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto
      • Ujenzi
      • Mazingira na Usafishaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mazingira na Mipango Miji
      • UKIMWI
      • Maadili
      • Ustawi wa Jamii
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Viombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

Dc Kibaha akabidhi gari jipya Divisheni ya ardhi na Mipango miji, awataka maafisa ardhi kutatua changamoto za wananchi,

Posted on: December 1st, 2025


 Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mhe. Nickson Simon, amekabidhi rasmi gari jipya kwa Divisheni ya Ardhi na Mipango Miji, lengo likiwa ni kuongeza ufanisi na kuwafikia wananchi kwa haraka zaidi katika utatuzi wa changamoto za ardhi.


Makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kibaha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.


Akizungumza wakati wa kukabidhi gari hilo, Mhe. Simon alisema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameweka kipaumbele katika utatuzi wa migogoro ya ardhi na upatikanaji wa maeneo ya viwanda na uwekezaji.


“Hili gari limeletwa ili muweze kuwafikia wananchi kwa haraka na kuhakikisha changamoto za ardhi zinatatuliwa kwa wakati. Nawaomba mlitunze na mlitumie kwa kazi iliyokusudiwa,” alisema Mhe. Simon, huku akimpongeza Mkurugenzi wa Manispaa, Dkt. Rogers Shemwelekwa, kwa kutekeleza maagizo kwa ufanisi.


Awali, akiwasilisha taarifa fupi, Dkt. Shemwelekwa alibainisha kuwa gari hilo linathamani ya shilingi milioni 170, na litakuwa nyenzo muhimu katika kuongeza kasi ya utoaji huduma bora hususan katika Divisheni ya Ardhi.


Kwa upande wake, Mkuu wa Divisheni ya Ardhi, Denis Kahumba, amesema changamoto ya usafiri ambayo ilikua ikikwamisha utendaji sasa imepatiwa ufumbuzi.


“Ahadi yangu ni kutoa huduma bora zaidi kwa wananchi. Tunashukuru kwa vitendea kazi na mazingira mazuri ya kazi ambayo yameongeza morali kwa watumishi,” alisema Kahumba.


Naye, Kamishna Msaidizi wa Ardhi Mkoa wa Pwani, Rugambwa Banyikila, ametoa pongezi kwa uongozi wa Manispaa ya Kibaha kwa kutatua changamoto zilizokuwa zikikabili ofisi ya ardhi na kuwataka watumishi kuongeza bidii na uwajibikaji.


Makabidhiano haya yanatarajiwa kuongeza kasi ya usimamizi wa ardhi, kutatua migogoro, na kuimarisha huduma kwa wananchi wa Kibaha, huku yakiendana na dira ya Serikali ya kujenga mazingira bora ya uwekezaji na maendeleo.

Matangazo

  • Tangazo la Kazi Halmashauri ya Manispaa Kibaha November 26, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUND VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 02, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -MSAIDIZI KUMBUKUMBU II October 06, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Dc Kibaha akabidhi gari jipya Divisheni ya ardhi na Mipango miji, awataka maafisa ardhi kutatua changamoto za wananchi,

    December 01, 2025
  • Dkt Bashiru awaagiza watendaji wa mifugo Kuongeza bunifu, Tafiti na Thamani ya Mazao

    November 28, 2025
  • KARIBU sana Kibaha

    November 16, 2025
  • DKR.Shemwalekwa afanya ziara ya kikazi kata ya Picha ya Ndege

    November 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

MUBASHARA RAIS DKT. SAMIA ANAWAAPISHA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI - NOVEMBA 18, 2025
Picha za Kutembea

Kiungo cha Haraka

  • Sheria Ndogo(Ushuru wa magari ya abiria na mizigo)
  • Barua Pepe
  • Uujazi wa Viwanja
  • Muundo Wa Kiuongozi Halmashauri
  • Dira na Dhamira ya Halmashauri

Kiungo Kinachohusiana

  • Mkoa wa Pwani
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Ofisi ya Raisi, Tawala za Serikali za Mikoa na Mitaa
  • Utumishi
  • Utumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Ramani Ilipo

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera za Siri
    • Disclamer
    • MMM
    • Sitemap
    • Huduma

Haki Zote Zimahifadhiwa