Tanga, Agosti 24, 2025
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Dkt. Rogers Shemwelekwa, ameungana na wanamichezo wa Halmashauri hiyo walioko jijini Tanga kwa ajili ya mashindano ya michezo ya SHIMISEMITA, ambapo amewatembelea na kuwahamasisha kuendelea kufanya vizuri katika michezo iliyobaki.
Dkt. Shemwelekwa amefika katika viwanja vya Hobbers Club, Tanga, ambapo ameshuhudia mchezo wa netiboli kati ya timu ya wasichana ya Manispaa ya Kibaha na Kakonko DC ambapo timu ya Manispaa ya Kibaha imeshinda.
Baada ya mchezo huo, amepata fursa ya kuzungumza na wanamichezo hao, akiwapongeza kwa juhudi walizofanya hadi sasa na kuwatia moyo kuendelea kupambana kwa ari na nidhamu ili kuiwakilisha vema Manispaa ya Kibaha.
“Nawapongeza kwa moyo wa ushindani na mshikamano mnaouonesha. Michezo ni sehemu muhimu ya kujenga afya, mahusiano na hata kuitangaza vyema Halmashauri yetu. Endeleeni kujituma, bado michezo mingine ipo mbele yetu,” amesema Dkt. Shemwelekwa.
Aidha wanamichezo wamempongeza Kwa kuwajali na kuahidi kushinda katika mashindano mbalimbali.
Mashindano hayo yanaendelea jijini Tanga yakihusisha halmashauri mbalimbali kutoka mikoa tofauti nchini.
Haki Zote Zimahifadhiwa