Na Mwandishi wetu
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi yaútalii Tanzania (TTB), Bw.Damasi Mfugale amekutana na Waheshimiwa Mabalozi na kuwakabidhi vitendea kazi vinavyotumika kutangaza utalii wa Tanzania kidijitali pamoja na kujadili mkakati wa kushirikiana katika kutangaza utalii wa Tanzania.
Mabalozi hao waliyoteuliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuiwakilisha Tanzania katika nchi za Omani, Austria, Namibia na Ufaransa wamepata elimu kuhusu utalii wa Tanzania pamoja na fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii zilizopo nchini.
Mabalozi waliyohudhuria kikao hicho ni Balozi wa Tanzania nchini Austria, Mhe. Balozi Naimi sweetie Hamza Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa, Mhe.Balozi Ali Mwadini, Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe.Balozi Fatma Mohammed Rajab na Balozi wa Tanzania nchini Namibia, Mhe. Balozi Ceaser Waitara.
Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 24/8/2023 katika ofisi ya Bodi ya Utalii Tanzania
Haki Zote Zimahifadhiwa