Na Byarugaba Innocent
Chanjo ya Polio awamu ya nne inatarajiwa kutolewa kuanzia 1 - 4 Desemba,2022 walengwa wakiwa ni watoto wenye umri wa miaka 0 hadi 5.
Zaidi ya watoto 98,000 wanategemewa kupatiwa matone ya kuzuia ugonjwa huo*
Mratibu wa Chanjo wa Halmashauri ya Mji Kibaha Hope Rutatina ameeleza kuwa kampeni hii itafanyika nyumba kwa nyumba, kwenye taasisi pamoja na kwenye vituo vya kutolea huduma za afya na kwamba chanjo hiyo haina madhara*
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dr. Tulitweni Mwinuka amewaasa Wazazi kuwatoa watoto wao ili kupatiwa chanjo ya kuzuia Ugonjwa wa kupooza ghafla ( Polio) ambao huwa na madhara makubwa ikiwemo kuziingiza familia kwenye gharama kubwa za matibabu
Akifungua kikao cha PHC,Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Renitha Ruzabico ametoa rai kwa Wazazi kutoa ushirikiano kwenye timu ya kufanikisha chanjo hiyo ili zoezi hili muhimu kwa Taifa liweze kufanikiwa kama linavyotarajiwa.
Ikumbukwe kuwa Mtoto asiyepata chanjo ni hatari kwa maisha yake na jamii inayomzunguka sababu anaweza kuambukizwa Magonjwa na kuambukiza wengine
Haki Zote Zimahifadhiwa