Na Byarugaba Innocent,Kibaha
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Nickson Simon leo Aprili 11,2023 anatarajia kuendelea na ziara kwenye Kata ya Tangini na Mailimoja ikiwa ni utaratibu wake wa kuwafikia wananchi kusikiliza na kutatua kero zao.
Katika msafara wake ataambatana na Wataalam kutoka Halmashauri ya Mji Kibaha na wengine kutoka taasis wezeshi zinazowahudumia wananchi kwa karibu ikiwemo Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO),Wakala wa Barabara na Mjini (TANROAD),wakala wa Barabara za Vijijini (TARURA) na DAWASA.
Kando ya kero za Wananchi,Mhe.Simon anatembea na agenda nne za Maendeleo ambazo ni Elimu,Mikopo ya asilimia 10,Usalama wa raia na Mali zao pamoja na Unyanyasaji wa watoto ambayo imekuwa tishio kwa siku za hivi karibuni. Elimu
Katika Elimu Mhe.Simoni tayari ameshaweka mikakati ya kuongeza ufaulu kwa kufuta alama sifuri ambapo amemwelekeza ofisa Elimu Sekondari Rosemary Msasi kuwapa malengo walimu ili waweze kufikia lengo hilo huku akielekeza na wazazi nao kuwajibika.
DC Simoni amesema sio vyema wazazi kuendeleza ushabiki wa mipira kwa kununua jezi ama kuendeleza urembo ili hali watoto wao hawajawawekea malengo kielimu badala yake watoto wanakosa hamasa ya kupenda kusoma kwenye ngazi ya familia.
Ametumia muda huo kuwashauri wazazi kuwapa ratiba za kujisomea watoto wao na kufuatilia utekelezaji huku akitoa rai ya kuhakikisha watoto hawasomi ilhali wakiwa na njaa shule.
Haki Zote Zimahifadhiwa