• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Kibaha Town Council
Kibaha Town Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Mji Kibaha

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhamira na Dira
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Kiutawala
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Usimamizi
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto
      • Ujenzi
      • Mazingira na Usafishaji
    • Vitengo
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha TEHAMA na Uhusiano
      • Ugavi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mazingira na Mipango Miji
      • UKIMWI
      • Maadili
      • Ustawi wa Jamii
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Viombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha

KONGAMANO LA MADINI LIMEONGEZA FURSA SEKTA YA MADINI

Posted on: May 11th, 2023

Wizara ya Madini imeagizwa kukagua Tozo na Kodi kandamizi

Serikali inaendelea kuboresha mazingira mazuri ya biashara ya madini

Tito Mselem na Mwanahamisi Msangi na Godwin Masabala, Mwanza

Wachimbaji wadogo wa madini wameshauriwa kulitumia Kongamano la wachimbaji wadogo wa Madini kama fursa ya kujiongezea tija na kujipatia kipato cha mtu mmoja mmoja kupitia mafunzo waliyopata.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa kwenye kilele cha Wiki ya Maonesho ya Madini wakati akifungua Kongamano la Wachimbaji Wadogo wa Madini na Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Wachimbaji Wadogo wa Madini Tanzania (FEMATA) uliofanyika katika ukumbi wa Rock City Mall …

[11:02 AM, 5/11/2023] +255 621 213 446: MAJALIWA AZITAKA HALMASHAURI KUSHIRIKISHA WACHIMBAJI UANDAAJI WA SHERIA NDOGO

*Asema katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2022/2023 mchango wa sekta ya madini ni asilimia 9.6

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezielekeza halmashauri zote za wilaya na miji, kwenye maeneo yenye madini ziandae sheria ndogo (by-laws) kwa kushirikiana na wadau katika sekta ya madini ili ziendane na Sheria ya madini.

Ametoa agizo hilo leo Jumanne (Mei 09, 2023) wakati akifungua Kongamano la Wachimbaji  Madini na Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA) kwenye ukumbi wa Rock City Mall jijini Mwanza

“Wakurugenzi wa Halmashauri wekeni mifumo bora ya kuweka tozo hizo na kuondoa kero kwa wachimbaji wadogo, punguzeni utitiri wa tozo kwa kubuni vyanzo vingine mapato”

Amesema kuwa Serikali inaendelea na jitihada za kuweka mazingira bora katika sekta ya uchimbaji mdogo na tayari imeshaanza kufanya marekebisho ya baadhi ya Kanuni na Sheria ya Madini na kuboresha mazingira ya biashara.

“Lengo la kufanya haya yote ni kuwezesha wananchi hasa wachimbaji wadogo nchini na wadau mbalimbali kushiriki ipasavyo katika uchumi wa madini”

Akizungumza kuhusu mchango wa Sekta ya madini kwenye pato la Taifa Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa umeongezeka kutoka asilimia 4.4 mwaka 2017, hadi asilimia 7.2 mwaka 2021. “Pia katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2022/2023 mchango wa sekta ya madini ni asilimia 9.6”

Amesema kuwa Serikali kupitia sekta ya madini imeweza kukusanya shilingi bilioni 409.66 sawa na asilimia 85.43 ya lengo la mwaka la kukusanya shilingi bilioni 479.51 katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2022/2023.

Kadhalika Mheshimiwa Majaliwa  ameiagiza Wizara ya madini kuharakisha mchakato wa kutafuta ufumbuzi wa suala Madini ya Lithium mapema iwezekanavyo ili kuweka wazi viwango vya uongezaji thamani kwa madini hayo kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali imeendelea kutenga maeneo kwa ajili ya wachimbaji wadogo na kurasimisha maeneo yenye milipuko ya madini ambapo katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Machi, 2023 zimetolewa jumla ya leseni 6,381, zikiwemo leseni 3,865 za uchimbaji mdogo wa madini (PML), leseni 1,649 za biashara ndogo ya madini (Brokers).

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali imeendelea kuhamasisha shughuli za uongezaji thamani madini ambapo hadi sasa jumla ya viwanda vitatu vya kusafisha wa dhahabu (Gold Refineries) vimeanzishwa .Viwanda vyote kwa pamoja vinauwezo wa kusafisha dhahabu kilogramu 515 kwa siku. Viwanda hivi vipo katika Mikoa ya Geita, Mwanza na Dodoma na vinafanya kazi”.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Madini Dkt. Stephen Kiruso amesema kuwa Sekta ya madini ni nguzo ya maendeleo duniani kote “Sekta hii imesaidia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa taifa na maendeleo ya mtu mmoja mmoja hapa nchini.

Amesema kuwa katika jitihada za kuikuza sekta ya wachimbaji wadogo, Serikali imetenga jumla ya maeneo 8 yenye ukubwa wa kilomita za mraba 112.29 kwenye mikoa ya Mwanza, Geita, Pwani na Shinyanga. “Wizara ya madini itaendelea kusimamia sekta hii kwa weledi ili malengo ya Serikali yafikiwe”

Naye Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA). amempongeza Rais Dkt Samia Sukuhu Hassan katika kuhakikisha anaisimamia vyema sekta ya madini ili iweze kuketa tija kwa uchumi wa nchi, wachimbaji na watanzania kwa ujumla

“Katika kipindi hiki cha Serikali ya awamu ya sita upatikanani wa maeneo na utoaji wa leseni za uchimbaji wa madini umeboresha, sisi wachimbaji wadogo mmetusikiliza, mmetusaidia mmetuheshimisha, alipo mama na wachimbaji tupo”

Matangazo

  • INEC yahimiza Wananchi mikoa 16 kujitokeza uboreshaji Daftari awamu ya pili May 14, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • TANGAZO KWA UMMA KUHUSU MIKOPO INAYOTOLEWA KWA VIKUND VYA WANAWAKE, VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU October 02, 2024
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -MSAIDIZI KUMBUKUMBU II October 06, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAADHIMISHO YA MIAKA MITANO YA HOSPITALI YA MJI KIBAHA

    June 27, 2025
  • WANANCHI KATA YA MBWAWA NA VISIGA WAPEWA ELIMU YA BIASHARA,NA UMUHIMU WA KODI KWA MAENDELEO,

    June 26, 2025
  • WATUMISHI WA HALMASHAURI YA MJI KIBAHA WAKIPEWA ELIMU YA MFUMO WA USAJIRI WA MAJENGO ODK

    June 20, 2025
  • HALMASHAURI YA MJI KIBAHA IMEVUNJA RASMI BARAZA LA MADIWANI JUNI 17,2025

    June 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

Mh. Waziri Mkuu akiwa ziarani Kibaha
Picha za Kutembea

Kiungo cha Haraka

  • Sheria Ndogo(Ushuru wa magari ya abiria na mizigo)
  • Barua Pepe
  • Uujazi wa Viwanja
  • Muundo Wa Kiuongozi Halmashauri
  • Dira na Dhamira ya Halmashauri

Kiungo Kinachohusiana

  • Mkoa wa Pwani
  • Sekretarieti ya Ajira
  • Ofisi ya Raisi, Tawala za Serikali za Mikoa na Mitaa
  • Utumishi
  • Utumishi Portal

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Free Visitor&Stat Counter

Ramani Ilipo

Wasiliana Nasi

Other Contacts

   

    • Sera za Siri
    • Disclamer
    • MMM
    • Sitemap
    • Huduma

Haki Zote Zimahifadhiwa