Na Byarugaba Innocent,Morogoro
Mradi wa shule Bora unaotarajiwa kuwa mwarobaini wa kuinua kiwango cha Elimu nchini uliozinduliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Vicky Ford Mwezi Aprili,2022 Mkoani Pwani upo mbioni kuanza utekelezaji wake.
Hayo yameelezwa na Mratibu wa mafunzo kutoka kutoka kwenye taasisi hiyo Ndugu Raymondi Kanyambo wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa Mawasiliano waliopo kwenye mamlaka za Serikali za mitaa na Wizara ya Elimu,Sayansi na teknolojia na taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo zinazotekeleza mradi huo yanayoendelea Mjini Morogoro kwenye Ukumbi wa Kingsway ili waweze kuhamasisha na kuhabarisha Umma kuhusu malengo na mafanikio ya kuanzishwa kwa mradi.
Kanyambo ameeleza malengo manne ya mradi huo kuwa ni kuimarisha ujifunzaji,ufundishaji,kutoa Elimu jumuishi na uimarishaji wa mifumo itajayowezesha kutoa Elimu stahiki kulingana na mahitaji ya wakati.
Aidha,ameongeza kuwa pamoja na kuwajengea uwezo walimu,mradi una lengo la kuona kuwa watoto wote wanaoanza Elimu ya awali wanafanikiwa kumaliza darasa la Saba na kuendelea na Elimu nyingine pasipokuwa na sababu za kimazingira isipokuwa kama watakatisha kwa sababu nyingine ikiwemo ugonjwa.
"Mradi unafanyakazi kwa karibu na Serikali hivyo utasapoti kuboresha na kuhuwisha mitaala ili iendane na wakati ikiwemo ya watu wenye ulemavu na kuimarisha mifumo ya ufundishaji kwa wadau kuanzia ngazi ya Taifa mpaka chini" amesema Kanyambo
Kwa upande upande wake mwakilishi kutoka OR-TAMISEMI Fred Kibano amewataka maafisa Mawasiliano kuendelea kufanyakazi zao kwa weledi za kutoa taarifa zao kwani kufanya hivyo ni kuwaunganisha wananchi na Serikali ambayo imekuwa ikipeleka Maendeleo mengi lakini hawahabarishwi ipasavyo
Aidha,Mkurugenzi msaidizi kutoka Idara ya Habari MAELEZO Rodney Thadeusi amewataka maafisa Habari wote kutoka kwenye Maeneo yote kuwasilisha miradi mikakati yote inayotekelezwa ili waweze kutambua na kupima ushiriki wao ili kama Kuna maeneo hawashirikishwi waweze kuwashauri makatibu Wakuu waboreshe eneo hilo kwani wananchi wanahitaji kupata taarifa sahihi za Serikali tena kwa wakati.
Mradi huu unatekelezwa kwenye mikoa tisa nchini utagharimu GBP 80 milioni sawa na fedha za kitanzania Bilioni 271
Wengine walioshuhudia uzinduzi kwa upande wa Tanzania ni Waziri wa Elimu,Sayansi na teknolojia Prof.Adolf Mkenda,Naibu Waziri OR-TAMISEMI Mhe.David Silinde,Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Abubakar Kunenge na viongozi wengine kutoa Wizara na Mikoa ya mradi
Haki Zote Zimahifadhiwa