Na Byarugaba Innocent, Pwani
Mkuu wa Mko wa Pwani Mhe. Abubakari Kunenge mwanzoni mwa wiki amekutana na uongozi wa shirika la Maendelo la Taifa - NDC kujadili namna Bora ya kuitangaza Kongane ya Viwanda inayomilikiwa na Shirika hilo iliyopo eneo la TAMCO halmashauri ya Mji Kibaha.
Mazungumzo hayo yaliyofanyika kwenye ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Aidha Mhe. Kunenge amemshauri Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Dkt.Nicolaus Shombe kuaandaa mchoro wa eneo hilo kwa ajili ya kulitangaza na kuwaleta wawekezaji wakubwa kwani lipo kimkakati hususan wakati huu ambao Serikali imejitanabaisha kwenye uwekezaji wa Viwanda kwenye Mkoa wa Pwani
“Ni wajibu wangu kuzisemea taasisi zote zilizopo mkoani kwangu, hivyo mnapaswa kuandaa mchoro wa eneo hilo, mnipatie ili tuweze kulitangaza kwa wawekezaji wanaotafuta maeneo ya uwekezaji,” alisema Kunenge.
Akifafanua faida za uwekezaji, Kunenge ameeleza kuwa unasaidia katika kufanisha malengo ya mkakati mkubwa wa mkoa wa kuongeza vyanzo vya mapato, hivyo eneo hilo la NDC ni muhimu na litasaidia kuongeza mapato kama atalisemea vizuri na likapata wawekezaji.
Katika Hatua nyingine Mhe. Kunenge amewapongeza watendaji wote wa Sekretarieti ya Mkoa na wa Halmashauri zote za Mkoa wa Pwani kwa utendaji wa kazi na kupelekea Mkoa kushika nafasi ya tatu nchini kwa kigezo cha makusanyo ya ndani ki asilimia
Aidha,Mkurugenzi mtenda wa shirika la Maendeleo ya Taifa NDC Dkt.Nicolaus Shombe amemshukuru mkuu wa Mkoa huo kwa kuweza kukutana nao na kufanya mazungumzo yenye tija kwa Taifa ya kuendeleza eneo hilo.
Dkt. Nicolas alifafanua kuwa Kongane la Viwanda TAMCO, Kibaha lina eneo ukubwa wa ekari 201.63 na limeteuliwa kujenga Viwanda katika Makundi matatu aliyoyataja kuwa ni Viwanda vya madawa na vifaa tiba, viwanda vya kuunganisha magari na mitambo pamoja na viwanda vya nguo.
Ameongeza kuwa eneo hilo linahitaji miundombinu ya barabara kama kilomita 4.8 na tayari Kilomita 1.6 imeshajengwa
Dkt.Nicholas alieleza kuwa tayari eneo hilo limepelekewa umeme wa Kv 33 na TANESCO huku miundombinu ya maji ikiwa inaendelea kuboreshwa.
Haki Zote Zimahifadhiwa