Halmashauri ya Mji Kibaha kupitia kitengo cha TEHAMA na Uhusiano inapenda kuwaelekeza watumishi ambao wanahitaji kupata Nakara ya mshahara ( Salary slip) kuwa zinapatikana kupitia Mfumo unaohitaji uwepo wa Mtandao:
I. Watumishi Portal:
- Jisajili katika mfumo wa utumishi “Watumishi Portal”. Katika mfumo huu utakuwezesha kupata taarifa zako za kiutumishi.
Vitu vya kuzingatia:
- Fahamu Majina yako kamili
- Hakikisha una barua pepe kama huna utalazimika kufungua
- Fahamu Check namba yako
- Ili kujisajili Bofya hapa.Kujisajili kwenye mfumo
II. Government Salary Slip Portal :
- Pia unaweza kupata stakabadhi yako ya mshahara kwa kutumia mfumo mpya wa "Government Salary Slip Portal" ambapo utahitajikia kujisajili kwenye mfumo.
Vitu vya kuzingatia:
- Check namba ya mtumishi
- Majina kamili kama yalivyo kwenye mfumo wa Rasilimali Watu yaani HCMIS maarufu kama Lawson.
- Tarehe ya kuzaliwa.
- Vote Code, Sub Vote Code, Namba ya Akaunti ya Benki unayopitishia mshahara.
- Fahamu pia Salary Scale, Salary Grade na Salary Step.
- Barua pepe (Email) inayofanya kazi.
i) Kwa mtumiaji wa mara ya kwanza lazima ujisajili kwanza; Ili Ujisajili Bofya https://salaryslip.mof.go.tz/Manage/EmployeeRegistration
ii) Kwa waliojisajili Tayari kwenye Mfumo “Government Salary Slip Portal” Bofya https://salaryslip.mof.go.tz/Account/Login?ReturnUrl=%2F
Kumbuka siku zote check namba yako ndio username yako. Hakikisha unauhakika na cheki namba yako.
Kwa maelezo zaidi tembelea ofisi za Utumishi Kibaha Mji
Haki Zote Zimahifadhiwa