Uwe na barua inayoenda kwa Mkurugenzi wa halmashauri ya mji iliyopitishwa na mtendaji wa mtaa na kata husika ikielekeza kuomba usajili wa kikundi. pia ionyeshe shughuli zinazofanywa na kikundi, idadi ya wanakikundi, muda kilipoanzishwa kikundi na namba ya simu ya kiongozi wa kikundi.
Uwe na mhutasari wa kikao cha wanakikundi uliojadili kuomba usajili ambao utaambatana na barua tajwa hapo juu.
Fika Ofisi ya Mkurugenzi kupitia idara ya Maendeleo ya Jamii ukiwa na pesa ya usajili Tshs. 10,000/= ambayo itatakiwa kulipwa kupitia akaunti ya NMB ambayo utapewa Ukifika Ofsini.