Na Byarugaba Innocent,Kibaha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ameendelea na Kasi yake ya kuimarisha miundombinu ya barabara na jumla ya Shilingi 1,887,001,200 zinajenga barabara ya lami Picha ya Ndege Bokotimiza kupitia kata ya Sofu
Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijiji na Mjini (TARURA) Kibaha Mhandisi Samwel Ndoveni amethibitisha kuwa fedha hizo zinatoka kwenye kapu la tozo ya Mafuta ambapo kipande cha awali chenye urefu wa 0.7 Kilometa chenye thamani ya Shilingi milioni 943,500,600 kimefikia asilimia 70 ya ujenzi.
Aidha,Mhandisi Ndoveni amesema kuwa Mhe.Rais Dkt.Samia ameidhinisha kipande kingine chenye urefu wa 0.7 Kilometa kwa gharama ya Shilingi 943,500,600 kujengwa ili kufikisha 1.4 Kilometa ambapo kandarasi ya ujenzi itasainiwa muda wowote ili kufikia mwanzo mwa 2024 kukamilisha vipande vyote viwili
Mhe.Mussa Ndomba ni Diwani wa Kata ya Sofu na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha amempongeza Mhe.Dkt.Samia na Serikali yake kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya barabara za Kibaha na kutoa rai kwa wananchi kuzitunza ili zidumu muda mrefu
Kandarasi ya ujenzi inafanywa na Kampuni ya M/S The Globallink General Contractors Ltd kwa miezi Saba kuanzia Machi 3,2023 tayari imeshakamilisha Makalavati yenye kipecho cha mm.1500 yenye urefu wa Mita 12,Makalavati yenye Kipenyo cha mm.1200 yenye urefu wa Mita 22,Makalavati yenye Kipenyo cha mm 900 yenye urefu wa Mita 48 na Makalavati ya Kipenyo cha mm 600 yenye jumla ya Kipenyo cha Mita 38 pamoja na ujenzi wa mitaro pembezoni mwa Barabara
"Mikakati ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya barabara ni kuendeleza miundombinu ya usafiri wa uhakika ili kusaidia Maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini"...amesema Protas Dibogo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha.
Haki Zote Zimahifadhiwa