Na.Byarugaba Innocent, Kibaha
Jumla ya timu nne kutoka kwenye halmashauri mbili za Wilaya ya Kibaha zimetinga hatua ya nusu fainali za mashindano ya Kombe la Samia yanayoendelea kwenye Viwanja mbalimbali yakilenga kuhamasisha wananchi kujiandaa kuhesabiwa kwenye zoezi la Sensa ya watu na Makazi linalotarajia kufanyika Agosti 23,2022
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Sara Msafiri amesema mashindano yameshirikisha jumla ya timu 16 kutoka kwenye kata 28 za Wilaya ya Kibaha huku yakisimamiwa na Chama cha Mpira wa Miguu-KIBAFA na yanaratibiwa kwa karibu na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na kwamba mpaka sasa yanakwenda vizuri kwani hakuna malalamiko yaliyojitokeza toka kwa timu Shiriki.
Mhe.Msafiri amewashukuru wadhamini wa mashindano hususan kampuni ya mafuta ya Afroil kama mdhamini Mkuu na mdhamini mwenza kampuni ya Tiper kwa kufanikisha kwani jumla ya jumla ya mipira 20, jezi jozi 13, Maji na juice zinazoendelea kutumiwa na wachezaji kwenye Michezo zimewezeshwa na wao
Aidha,Msafiri ameeleza kuwa mshindi wa mashindano hayo atapata fursa ya kwenda Ikulu kumkabidhi Kombe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake,mwakilishi wa Kampuni ya Afroil Abdul Karim Atiki ambao ndio wadhamini Wakuu wa mashindano hayo ametoa rai kwa makampuni mengine kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya Sita kwenye kazi za Kijamii hasa wakati huu wa kuhamasisha ushiriki w sensa ili kudhamini Michezo mingine kwani kufanya hivyo ni kurudisha shukurani kwa jamii,kuwaondoa Vijana vijiweni na kuzalisha wachezaji kama walivyoanza akina Mbwana Samatta ambao leo wanalipwa fedha nyingi lakini wametokea kwenye Michezo kama hii.
Katibu wa chama cha Mpira wa Miguu-KIBAFA Daudi Mhina amemshukuru Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya kwa kuanzisha mashindano hayo na kumtakia kheri ya mafanikio kwenye kuendelea na zoezi kuwahamasisha Wananchi wa Tanzania kwenye ushiriki wa Sensa itakafanyika Agosti 23,2022
Mashindano hayo yalizinduliwa rasmi Agosti 9 na yanatarajiwa kutamatishwa Agosti 21,2022
Haki Zote Zimahifadhiwa