Na.Byarugaba Innocent, Morogoro
Ikiwa ni siku ya hitimisho ya Maonesho ya nanenane Mwaka 2022 yenye kauli mbiu isemayo Agenda 10/ 30 Kilimo ni biashara; jiandae kuhesabiwa kwa Mipango bora ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Sara Msafiri na Waheshimiwa Madiwani wamefika kwenye banda la Halmashauri ya Mji Kibaha kujionea namna wakulima na wafugaji wanavyofanya shughuli zao ndani ya Wilaya.
Aidha,wamepata Elimu ya Kilimo cha Mjini,Ufugaji wa Mifugo pamoja na Samaki kwa kutumia teknolojia zinazoendana na Dunia ya leo.
Mkuu wa Wilaya Mhe.Sara Msafiri ameipongeza halmashauri ya Mji Kibaha kwa kutimiza takwa la kuwawezesha wajasiliamali kupitia asilimia 10 ya Mapato ya ndani ambao wanashiriki kwenye Maonesho wakiwa na bidhaa bora kabisa zinazotambulika kimataifa baada ya kutambuliwa Shirika la viwango nchini-TBS na kuwekewa msimbomilia.
Aidha, Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Kibaha Mhe.Mussa Ndomba pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii Mbegu Kambi Legeza wamefurahishwa na maandalizi pamoja na Maonesho yenyewe na kutoa rai kwa wananachi hususan wa Kibaha Mjini kuwa na desturi na kutembelea Maonesho hayo kwani yanaweza kuwaongezea maarifa mapya kwenye Kilimo na Ufugaji wa tija.
Wengine waliofika kwenye mahitimisho ya nanenane leo ni Katibu tawala wa Wilaya ya Kibaha Sozi Ngate, Mkurugenzi wa Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde, Wakuu wa idara pamoja na watumishi.
Maonesho ya 29 ya nanenane kanda ya Mashariki Mwaka 2022 yalionza rasmi Agosti 31,2022 yanatamatishwa leo na Waziri wa nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na uratibu Mhe.George Simbachawene
Haki Zote Zimahifadhiwa