HALMASHAURI YA MJI KIBAHA IMEVUNJA RASMI BARAZA LA MADIWANI JUNI 17,2025.
Halmashauri ya Mji kibaha limevunja Baraza Rasmi leo,Juni 17,2025 na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Katibu wa Wazazi wa Wilaya kibaha , Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mh, Nickson Saimon Pamoja na Wakuu wa Idara wa Halmashauri.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Musa Ndomba akizungumza katika kikao hicho amesema kuwa Kibaha Mjini imepata mafanikio makubwa yaliyopelekea Kibaha kuwa na Maendeleo.
Ndomba ,amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano tangu 2020 hadi 2025 Kibaha Mjini cha madiwani hao wamefanikiwa kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani kutoka Sh.bilioni 3.8 ya Mwaka 2020 mpaka kufikia bilioni 14 ya Mwaka 2024.
Ameongeza kuwa,katika kipindi cha mwaka 2024 /2025 mapato hayo yameongezeka zaidi ambapo mpaka sasa tayari wamekusanya kiasi cha Sh.bilioni 20 sawa na asilimia 200.
Aidha,Ndomba amesema kuwa kupitia mapato hayo Halmashauri kupitia Baraza la Madiwani wamefanikiwa kujenga Shule za Msingi 11 ambapo Kati ya hizo Shule tatu ni za mchepuo wa Kiingereza
Akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt . Shemwelekwa amesema kukamilika kwa miradi hiyo pia kumetokana na mchango mkubwa wa Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan ambaye amekuwa akitoa pesa nyingi kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
"Kipekee nawashukuru madiwani wote, Mbunge na Mkuu wa Wilaya kwa ushirikiano mkubwa uliokuwepo lakini shukrani hizi ziende kwa Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha nyingi ya kutekeleza miradi ya maendeleo,"amesema Shemwelekwa
Aidha ,Dkt.Shemwelekwa amewaomba Madiwani hao kwenda kuyasemea mafanikio yaliyopatikana katika kipindi chao kwa Wananchi ili kusudi waweze kupata nafasi ya kurudi katika uchaguzi mkuu.
Mbunge wa Jimbo la Kibaha Silvestry Koka ameungana na madiwani ,wakuu wa idara na watendaji wa Halmashauri hiyo kwa kazi kubwa na nzuri iliyofanyika ndani ya miaka mitano.
Koka,amewaomba watendaji na Wakuu wa idara kuendelea kushirikiana kikamilifu ili kusudi waweze kufanya kazi za kuhakikisha Halmashauri inaendelea Kusimama katika suala nzima la maendeleo .
Haki Zote Zimahifadhiwa