Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhe. Mussa Ndomba ameendesha Mkutano wa baraza la Madiwani robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2022/2023 ambao umefanyika siku ya Alhamisi tarehe 24 Mei, 2023 kujadili utekelezaji wa miradi ya Maendeleo na utoaji wa huduma kwa wananchi kwa kipindi cha miezi mitatu Januari-Machi
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhe. Selina Wilson Msenga amesema kuwa mpaka kufikia Machi, Halmashauri ya Mji Kibaha imekusanya Mapato ya ndani kiasi shilingi 3,536,459,030.00 sawa na asilimia 78 kati ya shilingi 5,552,561,120.00 zilizopangwa kukusanywa kwenye makisio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023.
Aidha, Mhe. Msenga ameeleza kuwa Halmashauri ya Mji Kibaha ilikadiria kukusanya jumla ya shilingi 45,809,511,506.43 kutokana ma mapato ya yatokanayo na ruzuku, mapato ya ndani na washirika wa maendeleo ambapo makusanyo ya kuanzia mwezi Julai 2022 hadi Machi 2023 jumla ya shilingi 29,993,221,804.05 sawa na asilimia 65.5 ya makisio ya Mwaka wa fedha 2022/2023 kimekusanywa
Mhe. Msenga ameeleza kuwa katika kipindi hicho, kiasi cha 26,322,286,642,05 sawa na asilimia 57 kimetumika kutolea huduma kwa wananchi ikiwemo kujenga miundombinu ya afya, elimu, pamoja na ununuzi wa vitendea kazi kwa watumishi
Kwa upande mwingine Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini Mhe. Silvestry Koka ameshiriki Mkutano huo ambapo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuidhinisha kiasi cha shilingi 1,280,400,000.00 kupitia mradi wa BOOST unatakaotekelezwa na idara ya elimu Msingi kwa kujenga shule mpya na kukarabati miundombinu ya shule kongwe kwenye Halmashauri ya Mji Kibaha
Aidha, Mhe. Koka amesema kuwa katika kuzithmini sekta za Afya na Elimu, fedha ya Mfuko wa Jimbo asilimia 80 huelekezwa kwenye Elimu huku asilimia 20 ikielekezwa kwenye sekta ya afya
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe. Simon Nickson John ambaye ni Mgeni Mwaliko kwenye Mkutano huo amewawapongeza watendaji wa Halmashauri ya Mji Kibaha wakiongozwa na Mkurugenzi Mhandisi Mshamu Munde kwa ushirikiano na kazi nzuri wanayoifanya ili kufikia Malengo ya serikali ya kutoa huduma stahiki kwa wananchi.
Aidha, ametumia fursa hiyo kuwashukuru kwa dhati namna walivyoshiriki kwenye maandalizi, Mapokezi na kushiriki kikamilifu mwanzo mpaka mwisho wa sherehe za Mbio za Mwenge wa Uhuru uliokimbizwa kwenye halmashauri ya Mji Kibaha tarehe 18 Mei,2023
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Mji Kibaha
25/05/2023
Haki Zote Zimahifadhiwa