Na Byarugaba Innocent,Kibaha.
Ikiwa ni siku chache kabla ya kuanza zoezi la umilikishaji rasmi wa Viwanja kwa wananchi walioingia kimakosa kwenye eneo la Halmashauri ya Mji Kibaha linalounganisha mitaa ya Kidimu, Mkombozi na Lumumba Kata ya Pangani leo Oktoba 21,2022 Kamati ya fedha na Utawala imefika kujionea hali ya utekelezaji wa Mradi.
Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Mussa Ndomba imeridhishwa na hali ya utekelezaji kwani tayari wataalam wameshapima Viwanja 12,066 kati ya Viwanja 16,750.
Akitoa taarifa Kaimu Mkuu wa Idara ya Mipangomiji na Ardhi Denis Festo amesema Kidimu vimepimwa Viwanja 4450,Mkombozi 6600 huku Lumumba vikipimwa Viwanja 1016 na kazi inaendelea.Aidha,tayari miundombinu ya ipo na inaendelea kuwekwa kwenye Maeneo yaliyosalia.
Katika kutimiza kazi ya umilikisha kwa kauli moja kamati imetoa rai kwa wananchi kuendelea na utaratibu wa kufika Ofisi za Halmashauri ili kupata gharama halisi ambazo kila mmoja atapaswa kulipia kutokana na Ukubwa wa eneo lake.
"Zoezi hili limeanza wiki mbili zilizopita,ilikuwa liwe limeshakamilika,hata hivyo kamati inaongeza wiki mbili nyingine kwa zoezi hilo baada ya hapo,Viwanja vitawekwa sokoni kuwauzia wananchi wengine wenye uhitaji"
Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Mji Kibaha ilikopeshwa fedha kiasi cha shilingi 1,588,000,000.00 kutoka Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa kupanga,kupima na kumilikisha kwenye mitaa tajwa hapo juu kama mamlaka ya upangaji baada ya kupewa eneo hilo na Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
Haki Zote Zimahifadhiwa