KIBAHA MANISPAA YANG'ARA UKUSANYAJI MAPATO
HALMASHAURI ya Mji Kibaha chini ya Mkurugenzi wake Dkt.Rogers Shemwelekwa imefanikiwa kupandisha mapato yatokanayo na ushuru wa huduma (Service Levy)kutoka Sh.milioni 420 mpaka kufikia Sh.bilioni 1.4.
Taarifa ya ukusanyaji wa mapato hayo imetolewa na mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Shemwelekwa katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi leo Aprili 29,2025 kikilenga kubainisha mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka 2020)2025.
Kikao hicho cha aina yake kilichofanyika katika Ukumbi wa Kibaha Shopping Mall licha ya kuhudhuriwa na Madiwani hao lakini pia kiliwashirikisha watumishi mbalimbali wakiwemo Watendaji Kata na walimu.
Akizungumza katika Kikao hicho mkurugenzi huyo amesema kuwa mapato ya ushuru wa huduma za jamii yameongezeka kutokana na kuweka mipango madhubuti ikiwa pamoja na kuunda timu maalum ya ufuatiliaji.
Dkt.Rogers amesema kuwa aliteuliwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan Machi 9,2024 kuwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha na alipofika alikuta ukusanyaji wa mapato yanayotokana na ushuru wa huduma za jamii( Service Levy) kiasi cha Sh.milioni 420 lakini mpaka sasa mapato hayo yamepanda mpaka kufikia Sh .bilioni 1.4.
Haki Zote Zimahifadhiwa