Na Byarugaba Innocent
Halmashauri ya Mji Kibaha imeendelea kufanya vizuri katika matumizi ya fedha za Serikali baada ya kupokea taarifa ya ukaguzi wa hesabu za halmashauri kwa Mwaka wa fedha 2020/2021 kutoka kwa mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Serikali inayoonesha hati Safi.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde kwenye kikao cha baraza la Madiwani kilichoketi Tarehe 16/06/2022 kujadili hoja za ukaguzi huku kikihudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Aboubakar Kunenge.
Kunenge ameipongeza halmashauri kwa kupata hati Safi na kutaka iendane na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha,ameongeza kuwa Wakuu wa Idara na vitengo kuwafanya kazi kwa vipaumbele na kujiwekea mikakati ikiwemo kudhibiti uvujaji wa Mapato na kurahisisha ulipaji wa Mapato kwa njia nyepesi
Kunenge ameongeza kuwa Halmashauri ibuni vyanzo vingine vya Mapato ili kupata fedha na kwamba sio mbaya kwa Halmashauri kama taasisi kufikiria kibiashara huku akitoa rai kwa Waheshimiwa Madiwani kujifunza uchumi na masoko kwa ajili ya kupanua wigo wa Mapato
Katika hatua nyingine ametoa maagizo ya kufunga hoja zilizomo kwenye uwezo wa halmashauri kabla ya tarehe 30 Juni 2022,kuwajibishwa kwa aliyesababisha hoja kwa kufuata taratibu za kisheria na kukamilisha kwa miradi inayoendelea.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mussa Ndomba amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa hotuba nzuri na kwamba kazi iliyobaki ni utekelezaji.
Haki Zote Zimahifadhiwa