Na Byarugaba Innocent,Kibaha
Jumamosi Septemba 16,2023 Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Mhe.Nickson Simon John amewaongoza mamia ya Wananchi kuadhimisha siku tlya usafishaji kwa kufanya usafi kwenye Soko la Loliondo kuanzia Saa 12 hadi saa 4 Asubuhi.
Pamoja na Mambo mengine Mhe.Simon ametoa rai kwa wananchi kuwa na utamaduni wa kufanya usafi kwenye Makazi yao pamoja na sehemu za biashara ili kuimarisha ustawi wa afya zao kwani uchafu na chakula hayaendani
Asumpta Maziku ambaye ni mfanyabiashara wa nguo kwenye Soko hilo amewakumbusha wenzake kujiwekea utaratibu rafiki wa kusafisha Mazingira kwani uwepo wa Mazingira machafu huwakimbiza hata wateja kwa kuhofia kuhatarisha afya zao
Mwenyekiti wa Mama lishe Sauda Hassan amesema kuanzia Sasa Mama lishe wataanza kutekeleza zoezi la usafi kwa vitendo ambapo kila Mama lishe atapaswa kuwa na vyombo maalum vya kuhifadhia taka huku Mkuu wa Wilaya akiwataka wote ambao hawataweza kwenye falsafa ya usafi kuwapisha wengine wanaoweza kuendelea kujitafutia riziki eneo Hilo ambalo limeajiri akina Mama wengi.
"Wasiofanya usafi usafi wataondolewa,ni jambo la kusikitisha Sana,tena la aibu kwa sehemu ya Chakula kuwa chafu.Mama lishe asiyeweza kwenda na kasi ya usafi,atupishe"alisema Mhe.Simon
Aidha,Mhe Simon ametoa wito kwa Mkurugenzi kuhakikisha Sheria ndogondogo zinaimarishwa hasa faini za ukusanyaji taka,uzoaji,ulipiaji na upelekaji dampo ili kuendana na wakati wa Sasa na kuimarisha kwa misingi ya usafishaji Mazingira
Haki Zote Zimahifadhiwa