Na Byarugaba Innocent,Kibaha.
Jumla ya wanafunzi 4358 wa Kidato cha pili wavulana wakiwa 1956 na wasichana 2402 katika Halmashauri ya Mji Kibaha wanatarajia kuhitimisha mtihani wa Taifa wa Upimaji Leo Novemba 10,2022
Kwa mujibu wa Afisa Elimu taaluma wa Halmashauri ya Mji Kibaha Edward Jidamva amesema Wanafunzi hao wanaojumuisha shule 40 kati yake za Serikali zikiwa 16 na binafsi 24 walianza Mtihani wao Oktoba 31,2022 wakiwa kwenye mikondo 135 watahitimisha leo Novemba 10,2022
"Tunashukuru sana wanafunzi wote wapo Salama kiafya na timamu na wanaendelea vema,tunamwomba Mwenyezi Mungu awaongoze wamalize salama"alisema na kuongeza
Aidha,Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari Rosemary Msasi ametoa rai kwa wanafunzi hao kukaa nyumbani kwa utulivu pindi watakapokuwa wanasubiri Matokeo yao ya kuingia kidato cha tatu huku akiwasihi kutojiingiza kwenye makundi yenye mienendo mibaya.
Halmashauri ya Mji wa Kibaha ni Miongoni wa Halmashauri tisa za Mkoa wa Pwani ambazo leo zitahitimisha Mtihani huo wa Upimaji kwa kufanya Somo la Maarifa ya nyumbani na Elimu ya Michezo.
Haki Zote Zimahifadhiwa