Na Byarugaba Innocent,Kibaha.
Shirika la Korea Foundation for International Health Care (KOFIH) limeiwezesha Halmashauri ya Mji Kibaha kupitia Idara ya Afya kiasi cha shilingi 263,346,400 kwa ajili ya kuiboresha Idara hiyo.
Akiwasilisha taarifa kwenye kikao cha Kamati ya fedha ya Mapokezi ya fedha Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt.Tulitweni Mwinuka amesema milioni 197,458,000 zitatumika kununua gari la Wagonjwa,Milioni 47,370,000 zitatumika kutolea Mafunzo kwa watoa huduma,huku kiasi cha milioni 11,925,000 zitatumika kutolea Mafunzo kwa Vijana balehe.
Aidha,Dkt.Tulitweni ameongeza kuwa damu salama itatumia kiasi cha shilingi 2,750,000 huku huduma ngazi ya jamii ikitumia shilingi 3,843,000.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha amekiri kupokea fedha hiyo na kwamba utaratibu wa matumizi unaandaliwa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhe.Mussa Ndomba amewashukuru wadau hao wa Maendeleo kwa namna wanavyoshiri kuchangia utoaji wa huduma hizo hivyo ametoa baraka za matumizi kwa malengo yaliyokusudiwa.
Haki Zote Zimahifadhiwa