Na Byarugaba Innocent, Morogoro
Mafunzo ya siku tatu yaliyokuwa yakifanyika kwenye Ukumbi wa Kingsway Mjini Morogoro yakiwapika maafisa Mawasiliano wa serikali kuhusu kutoa taarifa za mradi wa shule Bora na Miradi mingine ya kimkakati yamefikia tamati Jana tarehe 22 Septemba,2022
Programu ya Shule Bora ni mradi wa Serikali ya Tanzania wa kuboresha Elimu ya Msingi unaofadhiliwa kwa msaada wa UKaid wa Uingereza huku washirika wa utekelezaji wakiwa ni Cambridge education,Plan International,ADD International,Rescue committee kwa kusaidiana na OR-TAMISEMI kwa pamoja na Wizara ya Elimu ya juu,Sayansi na teknolojia.
Mkurugenzi msaidizi wa Idara ya habari-MAELEZO Rodney Thadeus ameeleza kuwa mafunzo haya yalikuwa yanaongeza maarifa waliyonayo wahudhuriji ametoa rai kwa maafisa hao kuwajibika kwa kuongeza ubunifu na uthubutu wa kutoa taarifa za Maendeleo ikiwemo kupiga picha za utekelezaji kwa namna Serikali inavyotatua changamoto za wananchi wake na kutolea ufafanuzi wa taarifa za upotoshaji zinatolewa na wachache wasioitakia mema nchi yetu
Aidha,Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini OR-TAMISEMI, Angela Msimbila amewapongeza wahudhuriaji wote wa mafunzo hayo ambayo yamewapa mwanga na Chachu ya mabadiliko ya kuandika na kutoa taarifa za miradi yote inayotekelezwa kwenye Maeneo yao ikiwemo shule Bora kwani wakati huu wananchi wanahitaji kuhabarishwa kwa njia tofauti ikiwemo mitandao ya Kijamii ambako Dunia ipo Sasa
Raymond Kanyambo,mratibu wa mafunzo kutoka Cambridge Education amesema kuwa kitendo cha kutamatisha mafunzo ni kiashiria cha kwenda kufanya kazi za kuhabarisha Umma juu ya malengo na dhamira ya mradi hivyo wafadhili wanatarajia kuona taarifa nyingi zitakazohamasisha ushirikiano chanya kwenye utekelezaji kati ya wafadhili,Serikali na jamii ili mradi uwe na tija.
Mradi wa Shule Bora unashirikisha Mikoa tisa nchini kwa lengo la kuinua kiwango cha Elimu ulizinduliwa Mkoani Pwani Aprili 4,2022 na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Mhe.Vicky Ford.
Haki Zote Zimahifadhiwa