Katika maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019, Halmashauri ya Mji Kibaha pamoja na mambo mengine imetoa elimu ya Uchaguzi kwa Wadau wa Uchaguzi pamoja wananchi kwa ujumla wake.
Lengo la Elimu hii ni kuhamasisha wananchi kujitokeza kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 muda utakapowadia.
Aidha, wananchi wanahamasishwa kujisajili kwenye rejesta za wakazi ili kuwezesha takwimu zitakazorahisisha kuendelea na maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Ili kuhakikisha lengo hili linatimia Halmashauri imeshirikisha wadau mbali mbali wa Uchaguzi kupitia kikao cha Wadau wa Uchaguzi kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kibaha 01/07/2019 ambapo waadau walioshiriki kikao hicho ni pamoja na Mwakilishi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kibaha, Maafisa Tarafa, Viongozi wa vyama vya Siasa, Viongozi wa dini, Viongozi wa Asasi za Kiraia, Watu Maarufu, TAKUKURU, Jeshi la Poilisi, Wasanii pamoja na Wanahabari.
Mikutano ya wananchi na vikao vya wadau wa Uchaguzi imeendeshwa kwenye kata zote 14 za Halmashauri ya Mji Kibaha ambako mabango na vipeperushi vya elimu ya Uchaguzi vimesambazwa.
Haki Zote Zimahifadhiwa