Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 04, 2023 ameshiriki sherehe za uapisho za Rais mteule wa Zimbabwe Mheshimiwa Emmerson Mnangagwa zilizofanyika katika uwanja wa Harare, Zimbabwe.
Mheshimiwa Rais Mteule Mnangagwa ameshinda uchaguzi huo kwa kura zaidi ya milioni 2.3 kati ya kura milioni 4.4 zilizopigwa sawa na asilimia 52.6 dhidi ya mpinzani wake Nelson Chamisa ambaye alipata kura milioni 1.9 sawa na asilimia 44.
Ushindi huo unamfanya Mheshimiwa Mnangagwa kuongoza nchi hiyo kwa kipindi cha pili cha miaka mitano.
Mheshimiwa Majaliwa amemuwakilisha Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uapisho huo.
Haki Zote Zimahifadhiwa