Na Byarugaba Innocent Kibaha.
Mbunge wa Kibaha Mjini Mhe Silyvestry Francis Koka amekabidhi kiasi cha shilingi milioni 3 kwa walimu wa shule ya Sekondari Koka iliyopo Kata ya Sofu Wilaya ya Kibaha. Fedha hiyo imetolewa ikiwa ni ahadi aliyoitoka wakati akizindua shule hiyo Aprili, 2023 ili kuwapa motisha walimu. Hiyo si mara ya kwanza kwa Mbunge huyo kutoa motisha shuleni hapo kwani mwanzoni wa Mwaka huu 2023 Koka alitoa shilingi 500,000/- kwa walimu wa shuleni hapo.
Aliwasilisha fedha hiyo kwa niaba ya Mhe.Mbunge, Katibu wa Mbunge Method Mselewa amewaambia Viongozi, wazazi,na walimu shuleni hapo kuwa ana imani fedha hiyo itachochea ufundishaji
" Mhe Mbunge anatamani kuona shule hii pamoja na shule nyingine za Kibaha zinafanya vizuri kwenye ufaulu, na kwamba amedhamiria kuhakikisha walimu wanakuwa na mazingira mazuri ili nguvu yao waelekeze kwenye ufundishaji"... amesema Mselewa
Awali akimkaribisha Katibu wa Mbunge, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Sofu Mhe. Mussa Ndomba Diwani wa Kata ya Sofu amempongeza Mhe Koka kwa namna anavyoisaidia kata hiyo hususan.
"Mhe Koka ameshafanya mambo mengi hapa, alitoa eneo, akasaidia Ujenzi, ametoa madawati na kaniambia analeta na Mashine ya kupiga kopi na juzi tu tumemaliza kujenga kitako cha tenki la maji na tenki lipo tayari ameshatoa"
Akitoa shukrani kwa Mbunge, Mkuu wa shule hiyo Mwl Magreth William amesema, siku zote Mhe Koka amekuwa chachu ya ufanisi wa majukumu na uboreshaji wa mazingira ya kujifunza na kujifunzia shuleni hapo. Amemwomba aendelee kusaidia shule hiyo Ili iwe ya mfano wa kuigwa Kibaha.
Haki Zote Zimahifadhiwa