Na Byarugaba Innocent,Kibaha.
Siku hazigandi!Tayari ni miaka miwili tangu Mama aingie madarakani.Huyu ni Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Halmashauri ya Mji Kibaha imeungana na watanzania wengine kifua mbele kusherekea siku hizi 730 za ushindi kwenye sekta ya Afya.Tayari Bilioni 2,718,928,572 zimetumika kuboresha huduma za afya ili kuimarisha afya za Wananchi wake waweze kushiriki kwenye shughuli za Maendeleo na kuinua uchumi wa Taifa na kipato cha mtu binafsi
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde awali ya yote anamtakia afya njema Mhe.Rais ili aendelee kuwaongoza watanzania.
Mhandisi Munde ameeleza kuwa kati ya Machi,2021 mpaka Machi,2023 kiasi cha milioni 500 kimetolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa wodi tatu;Wanaume,wanawake na Watoto.
Aidha,Machi 2022 kiasi cha milioni 800 kimeongezwa kwa ajili ya ujenzi wa majengo manne;jengo la upasuaji wa watoto,Wanaume,wanawake pamoja na jengo la kuhifadhiaMaiti.Miundombinu yote hii imeongezwa kwenye hospitali ya Wilaya Lulanzi ili kupanua wigo wa huduma za kitabibu.Mnyonge mnyongeni,haki yake mpeni.Mama amefanya makubwa Sana.Atafanya zaidi!
Mhandisi Munde ameongeza kuwa Dkt.Samia katika kipindi hicho ametoa kiasi cha milioni 900 kujenga vituo viwili vya afya kwenye Kata za Pangani na Kongowe ili kuwapunguzia wananchi umbali mrefu waliokuwa wanatumia kufuata huduma za afya.Ameanza na majengo ya OPD,Maabara,upasuaji na vichomea taka.Anaupiga Mwingi!
Serikali ya Dkt.Samia imeendelea kuwajali wananchi wake kwa kuwashirikisha wadau wengine wa Maendeleo wakiwemo wananchi wenyewe kushiriki kwa kutoa nguvukazi,Halmashauri na TASAF ambapo kiasi cha Milioni 518,928,572 kimeweza kukamilisha zahanati tatu za Sofu,Saeni,Mwanalugali pamoja na kujenga nyumba ya watumishi wawili Mtaa wa Vikawe.
Philemoni Maliga Mwenyekiti wa Machinga Mkoa wa Pwani amesema kazi anazozifanya Mhe.Rais zinaonekana kwenye sekta nyingi ikiwemo afya hivyo amewaomba wananchi kumuunga mkono ili aendelee kutuletea Maendeleo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhe.Mussa Ndomba amemshukuru Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM-Taifa kwa kazi kubwa anayoifanya ya kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya 2020-2025.
Haki Zote Zimahifadhiwa