Na Byarugaba Innocent, Pwani
Mwekezaji Alghmlas Abdalah kutoka Reyadh nchini Saudi Arabia akiwa ameongoza na Balozi wa Tanzania nchini humo Mhe.Ali Mwadini amefika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani na kupokelewa na Mwenyeji wao Mhe.Abubakar Kunenge na kufanya mazungumzo ya tija yanayolenga uwekezaji nchini hususan,Mkoa wa Pwani.
Pamoja na Mambo mengine,Mhe.Kunenge amewakaribisha na kutumia wasaa huo hiyo kuwaeleza fursa zilizopo ndani ya Mkoa wa Pwani na kuwa hawajakosea kufikiria kuweza kwani ni Mahali sahihi kwa uwekezaji
Mhe.Kunenge amefafanua kuwa Mkoa una fursa nyingi za uwekezaji kwenye sekta ya Viwanda, Uvuvi, Kilimo,Utalii na Mifugo
"Mkoa wa huu ni eneo la kimkakati kwa uwekezaji kwani lipo jirani na Jiji kuu la Kibiashara la Dar-es-Salaam nchini Tanzania ambapo pia Kuna bandari ya kusafirishia bidhaa na kuingizia malighafi kutoka ughaibuni" amesema Mhe.Kunenge.
Aidha,Mhe.Kunenge amesema kuwa kuwa uwepo wa reli ya kisasa ya SGR,nishati ya umeme na Maji ya uhakika pamoja na uwepo wa Kongani kubwa ya Viwanda barani Afrika ya Sino Tan Kwala Industrial Park ni kichocheo kingine cha uwekezaji Pwani
Kwa upande wake Mhe.Balozi Ali Mwadini ameeleza kuwa amefika na mwekezaji huyo kuona fursa za kuweke kwenye machinjio za kisasa,unenepeshaji Mifugo,Kilimo cha kisasa,Viwanda vya kutengeneza vifungashio na kuwekeza kwenye sekta ya Utalii.
Mkoa wa Pwani bado una maeneo mengi ya uwekezaji ikiwemo Zegereni Kibaha Mjini,Kwala, Chalinze,Visegese,Chamakweza.Aidha,Kisarawe,Kibiti na Rufiji yapo maeneo yanayofaa kuwekeza.
Haki Zote Zimahifadhiwa