Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mary Chatanda, ameelezea kuridhishwa kwake na maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji Kibaha. Ziara yake ya kikazi ililenga kukagua Uterekezaji wa Ilani ya Ccm na Hatua zilizopigwa katika kuboresha huduma za Afya kwa wakazi wa Kibaha.
Chatanda alibainisha kuwa hospitali hiyo ina umuhimu mkubwa katika kuboresha upatikanaji wa huduma za Afya, hasa kwa Wanawake na Watoto.
Alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyostahili.
Hospitali ya Halmashauri ya Mji kibaha Imesaidia kuboresha Huduma ya Afya kwa Wananchi na Sasa wanapata Huduma za Matibabu kwa ukaribu bila kulazimika kusafiri umbali mrefu na imepunguza idadi ya vifo vinavyoweza kuzuilika.
Haki Zote Zimahifadhiwa