Na Byarugaba Innocent,Pwani
Naibu Waziri wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega ametembelea Maonyesho ya Uwekezaji na Biashara yanayoendelea kwenye Viwanja vya Stendi ya Zamani maili moja Mkoani Pwani.
Maonyesho haya yamezinduliwa Jana na Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt .Jakaya Mrisho Kikwete yakiwa na kauli mbiu isemayo;Pwani ni sehemu sahihi kwa uwekezaji,pamoja tujenge Viwanda kwa uchumi na ajira endelevu huku ikishirikisha kampuni,Mashirika na taasisi mbalimbali.
Mhe.Ulega ameridhishwa na Mpango kabambe wa Halmashauri ya Mji Kibaha wa kupanga,kupima na kutenga maeneo maalum ya uwekezaji wa Viwanda kwenye Kata za Visiga,Mbwawa na Pangani kuwa utaratibu huo ni mzuri kwani unarahisha upatikaji wa bidhaa lengwa
Awali alitembelea Banda la Wizara ya Ardhi,nyumba na Maendeleo ya Makazi ambapo alipata utaratibu wa namna Wizara hiyo inavyorahisisha utoaji wa hati kwa wawekezaji nchini.
Hata hivyo,ametoa rai kwa wataalam wa Wizara hiyo kuongeza Kasi ya upimaji wa maeneo ili kupunguza Migogoro ya Ardhi ambayo imeshamiri hasa Mkoa wa Pwani.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde amesema Kibaha itaendelea kupima maeneo na kuweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji kuja kuwekeza
Aidha,Mhe.Ulega ameridhishwa na pia na kiwanda cha Hester Bioscience Afrika limited kinachotengeneza chanjo za wanyama na kwamba kimekuwa Mkombozi kwa Serikali kwani badala ya kuagiza kutoka nje ya nchi Sasa zinapatikana hapa nchini
Aidha,ametoa rai kwa wananchi kuongeza Kasi ya Ufugaji ili kujiingizia kipato kuanzia ngazi ya familia ili kujikwamua na wimbi la umaskini kwa Sasa uhakika wa chanjo upo
Maonyesho haya ya Viwanda Mkoa wa Pwani yanafanyika kwa mara ya tatu yanatarajiwa kufikia tamati Oktoba 10,2022
Haki Zote Zimahifadhiwa