Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Rashid Mchata amewaasa watumishi katika ofisi yake kutekeleza majukumu yao katika hali inayoakisi uhalisia wa utumishi wa Umma.
Hayo ameyasema Julai 18, 2023 katika kikao chake na watumishi hao kwenye ukumbi wa mikutano wa jengo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kwa lengo la kufahamiana na kukumbushana wajibu na majukumu katika utumishi wa umma.
"Watumishi zingatieni nidhamu, kuwahi kazini, hudumieni wateja kwa lugha nzuri, kuvaa kwa unadhifu, na tabia zetu ziakisi heshima ya utumishi wa Umma kwani sisi ndiyo mabalozi wa Serikali," amesema.
Katika kikao hicho, watumishi wamepata fursa ya kutoa mawazo yao kwa lengo la kuboresha utekelezaji wa majukumu katika ofisi hiyo.
https://www.instagram.com/p/Cu3RJ93Ituh/?igshid=MTc4MmM1YmI2Ng==
Haki Zote Zimahifadhiwa