SERIKALI YA RAIS SAMIA YAMWAGA MABILIONI YA FEDHA KWA MIRADI KIBAHA MJI
Na Byarugaba Innocent, Kibaha
Halmashauri ya Mji Kibaha imepokea kiasi cha fedha jumla ya Shilingi 5,471,261,909.20 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya kutekeleza shughuli za Maendeleo pamoja na Matumizi mengine ikiwemo uendeshaji wa Ofisi
Mweka hazina wa Halmashauri y Mji Kibaha CPA Norah Mbendera amechangua kiasi kilichopokelewa kuwa ni fedha ya Miradi ya Maendeleo kiasi cha Shilingi 2,061,814,889.20, Malipo ya moja kwa moja (Dummy Payment) Shilingi 3,356,066,020 huku kiasi cha Shilingi 53,381,000. Ikiwa ni ruzuku ya Matumizi mengineyo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Dkt.Rogers Jacob Shemwelekwa amempongeza na kumshukuru Sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan na Serikali yake ya awamu ya sita kwa kutenga na kuidhinisha fedha hiyo kuhakikisha Miradi ya Maendeleo katika Sekta zote inakamilika kwa wakati na kuwanufaisha Watanzania hivyo ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa Wataalam kuisimamia kikamilifu ili Ujenzi wake uendane na thamani (Value for Money)
Fedha iliyopokelewa inakwenda kutumika kwenye Miradi ya Sekta ya afya, Utawala, Elimu, Biashara,pamoja na kulipa mishahara ya watumishi.
"Watumishi wenzangu tuna kila sababu ya kumshukuru na kumwombea afya njema Mhe.Rais wetu Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa Uongozi wake bora tena wa Vitendo.Akisema analeta hela anazileta hivyo kazi yetu ni kuzisimamia ili zifanye kazi iliyokusudiwa" amesisitiza Dkt.Rogers Shemwelekwa.
Haki Zote Zimahifadhiwa