SHULE YA KATA MWANALUGALI YAANZA KWA KISHINDO UFAULU KIDATO CHA SITA
Na.Byarugaba Innocent, KTC
Shule ya Sekondari Mwanalugali iliyopo Kata ya Tumbi halmashauri ya Mji Kibaha imeanza vema kwenye ufaulu wa matokeo ya kidato cha sita yaliyotangazwa Julai 5,2022 kwa kufaulisha wanafunzi wote 32 sawa na 100 asilimia.
Mkuu wa shule hiyo Joseph Mkumbo amesema wanafunzi walianza masomo yao 2020 wakiwa ni chaguo la pili lakini kwa juhudi za walimu na wanafunzi wenyewe waliweza kupambana kimasomo na Sasa matunda yameonekana kwa ufaulu wa kishindo.
Mkumbo ameeleza kuwa kati ya wanafunzi 32,23 wamepata daraja la pili,9 wamepata daraja la tatu huku shule ikiwa nafasi ya 27 kati ya shule 33 Kimkoa na Kitaifa ikishika nafasi ya 547 kati ya 644 kwa wastani wa G.P.A ya 3.1
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kibaha Eng.Mshamu Munde ameipongeza Idara ya Elimu Sekondari kwa usimamizi unaoleta tija kitaaluma.
Aidha,amewapongeza Walimu, Wazazi,jamii yote ya Mwanalugali na wanafunzi kwa jitihada zilizofanikisha matokeo hayo mazuri.
Marco Bahebe ambaye ni Katibu wa tume ya Utumishi wa Walimu Wilaya ya Kibaha amewapongeza Walimu kwa kufuata Sheria,taratibu na Kanuni za kiutumishi na kwamba huo ndio muarobaini wa mafanikio.
Shule hii ilianza kudahili wanafunzi Mwaka 2020 kwa tahasusi ya HGL hivyo huu ni uzao wake wa awali
Haki Zote Zimahifadhiwa