Akizungumza wakati akiongoza Ujumbe maalumu wa Tanzania nchini China Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknlojia Qs Omar Juma Kipanga (Mb) alisema Kuwa Serikali ya Tanzania inashukuru Sana Serikali ya Watu wa China kwa Kuisadia Tanzania kukua zaidi katika Sayansi na teknlojia kwa jamii hasa wanafunzi waliopo Shule na Vyuo vikuu vilivyopo ndani na nje vya Tanzania,
Ujumbe Huu wote uliopo hapa Unashukuru Sana kwa Kuwapo China Ili kuwakilisha Serikali ya Tanzania na Watu wake kwenu lengo la Kupata Mafanikio ya Ushirikiano baina ya watu wa Tanzania na China
Aidha Qs Kipanga alifafanua Kuwa TVET Technical and Vocational Education Training Itasaidia Jamiii ya Tanzania Kuwa mbali zaidi katika Teknlojia na Sayansi kwa kipindi kifupi mno Kutoka kwa Watu wa China,
"Ifike hatua lazima tulubali Kupata Elimu ya Sayansi na teknlojia Kutoka China kwa maslahi mapana ya Tanzania Ili jamii ipate Maendeleo makubwa alisema Qs Kipanga
"Mwisho TVET itakapokamilika Tanzania itakua Ni miongoni mwa nchi zenye Mafanikio ya Sayansi na teknlojia kwa kipindi kifupi mno ikiwa yote hii Ni jitihada za Rais Samia na Serikali yake ya Chama Cha mapinduzi ya kuhakikisha jamii inakua na Mafanikio ya Sayansi na Teknlojia alifafanua Qs Kipanga"
Ujumbe wa wazira ya Elimu Sayansi na Teknlojia Upo Nchini China Kwa Ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na China Na Ujumbe huo unaongozwa na Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia na Kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini China.
Haki Zote Zimahifadhiwa