Na Byarugaba Innocent, Pwani
Mfuko wa maendeleo ya Jamii nchini -TASAF kupitia programu ya mpango wa kunusuru kaya maskini umehawilisha jumla ya milioni 107,743,889 kwa walengwa 2499 wanatoka kwenye mitaa 60 kati ya 73 ya halmashauri ya Mji Kibaha.
Mratibu wa Halmashauri ya Mji Kibaha Anita Lyoka ameeleza kuwa milioni 22,091,041 zimelipwa taslimu kwa walengwa 546 huku milioni 85,652,848 zikilipwa kwa walengwa 1953 kwa njia ya mtandao kuanzia Julai 26-28,2022.
Fedha hizi hutolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia TASAF ili kuwanusuru walengwa na wimbi la umaskini ambapo hujikita zaidi kwenye kuwasomesha watoto na kugharamia matibabu ili kujikomboa na ujinga na Makazi.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Kibaha Mhandisi Mshamu Munde ametoa rai kwa walengwa kuzitumia fedha hizo kama Serikali inavyotarajia na kwamba wasitumie vinginevyo kwani lengo la Serikali halitafikiwa.
Athuman Mwela kutoka Mtaa wa Msangani na Asha Kola kutoka Mtaa wa Bungo wameshukuru Sana Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia mpango huo kwani fedha hizo zinawasaidia Watanzania wengi kugharamia mahitaji ya watoto shule kama Sare,Madaftari na hali hiyo imeboresha mahudhuria ya watoto shuleni hivyo ombwe la ujinga nchini limedi kupunguza
Aidha, TASAF kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani-UNICEF wametoa vifaa vya usafi wa mwili kwa wasichana balehe wanasoma wa kati ya miaka 10-18 wanatoka kwenye mpango wa kunusuru kaya maskini.
Anita amesema jumla ya boksi 1099 yamepokelewa yenye taulo maalum za kike, michw ya sabuni na ndoo na ugawaji kwa walengwa utafanyika baada ya taratibu kukamilika.
Haki Zote Zimahifadhiwa