Kamati ya Ujenzi Katika Ujenzi wa Majengo manne(Jengo la Mionzi, Jengo la kina mama/wazazi, Jengo la upasuaji na jengo la kufulia) ya kituo cha Afya Mkoani ambayo ilihusisha wanajamii na watumishi wakiwa katika kikao kazi cha kupitisha baadhi ya malipo ya ujenzi baada ya ukaguzi wa kina wa ujenzi.
Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi Mhandisi Brighton Kisheo alisema ujenzi mpaka sasa umefikia asilimia zaidi ya 98, aidha ametoa shukran za dhati kwa
kamati kwa ushirikiano ulionyeshwa na wanakamati hadi kufanikisha ujenzi huo kwa 98% mpaka sasa kwa majengo manne pia ametoa rai kwa watakao tumia majengo hayo kuwa watatakiwa kuyatunza majengo na miundombinu yote kwa faida ya vizazi vya sasa na vya baadaye.
Aidha Mjumbe wa kamati ujenzi kutoka kwenye jamii Ndg.William A. Swai Amesema Ujenzi wa majengo manne ya kituo cha afya
Mkoani umenda vizuri sana kutokana na ushirikishwaji wa wanajamii na watumishi wa Halmashauri kwani imeonekana waziwazi kuwa baadhi ya
wanajamii walikuwa na utaalamu na uzoefu katika kazi za ujenzi, hivyo basi ameshauri kuwepo na ushirikishwaji katika kazi nyingine za serikali ili kuleta ufanisi zaidi.
Haki Zote Zimahifadhiwa